Ncha ya anga
Ncha ya anga ni nukta angani pale ambako mstari wa kudhaniwa baina ya ncha za dunia (yaani mhimili wa mzunguko wa Dunia) inaelekea. Kwa mtazamaji Duniani inaonekana kama nyota zote zinazunguka ncha ya anga.
Kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia kuna nyota angavu ya Kutubu (en:Polaris) iliyopo karibu sana kwenye ncha ya anga ya kaskazini.
Kwenye nusutufe ya kusini hakuna nyota angavu kwenye ncha ya anga; σ Sigma Octantis iko karibu na hivyo wakati mwingine inaitwa « Polaris Australis » (nyota ya ncha ya anga ya kusini). Lakini Sigma Octantis haikupata umuhimu sawa kama Kutubu ambayo ni nyota inayoonyesha ncha ya anga ya kaskazini ikiwa ni nyota angavu zaidi ya mag 1.98 iliyotumiwa na mabaharia tangu karne nyingi kujua mwelekeo wa kaskazini. Kwenye nusutufe ya kusini mwa Dunia kundinyota la Salibu lilitumiwa zaidi kwa kusudi hili maana mstari mrefu wa msalaba wake umetokeza upande wa ncha ya kusini angani.
Marejeo
hariri- A Quick Guide to the Celestial Sphere, tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017