Nusutufe ya kaskazini

nusu ya Dunia ambayo iko kaskazini mwa ikweta

Nusutufe ya kaskazini (pia nusudunia ya kaskazini; Kiing.: Northern Hemisphere) ni nusu ya Dunia ilioko upande wa kaskazini ya ikweta.

Nusutufe ya Kaskazini: Amerika Kaskazini (kushoto) pamoja na sehemu ya juu ya Amerika Kusini, Eurasia (Asia na Ulaya) pamoja na kaskazini ya Afrika
Tofauti ya viwango vya bahari na nchi kavu kati ya nusutufe za dunia

Tofauti na nusutufe ya kusini hii kaskazini ya Dunia ina maeneo makubwa zaidi ya nchi kavu; theluthi mbili za nchi kavu za dunia ziko hapa kaskazini. Kwa hiyo pia sehemu kubwa ya binadamu hukaa kwenye nusutufe hii, ni asilimia 90 ya watu wote wanaoishi duniani.[1]

Kati ya mabara ni yote ya Ulaya, Asia na Amerika Kaskazini yaliyopo kwenye nusutufe hii.

Majira ya joto huwa ni hapa kuanzia Juni hadi Septemba, na majira baridi kuanzia Disemba hadi Machi.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Pretty Much Everyone Lives In The Northern Hemisphere , tovuti ya Business Insider ya May 4, 2012, iliangaliwa Agosti 2017