Ngano za Wenzi Watatu
Ngano za Wenzi Watatu (kwa Kilatini Legenda trium sociorum) ni kitabu muhimu zaidi kati ya vile visivyo rasmi vilivyoandikwa katika karne XIII kuhusu Fransisko wa Asizi. Kina sura 18.
Uandishi wake
haririKwa muda mrefu kilidhaniwa kuandikwa na wenzi watatu wa mtakatifu huyo, Anjelo, Leo na Rufino, hivyo wakati mwingine kilipewa kipaumbele.
Kadiri ya mtazamo huo, miaka ishirini baada ya kifo cha Fransisko hamu ya kujua habari zake ilikuwa imeongezeka ndani na nje ya shirika. Ndiyo sababu wakati wa mkutano mkuu wa mwaka 1244 mtumishi mkuu mpya aliagiza ndugu wote walete kwa maandishi kumbukumbu yoyote waliyonayo juu yake. Kutokana na agizo hilo kitabu hicho kilitungwa katika miaka 1241-1247 kikaitwa “Ngano za Wenzi Watatu”. Kinategemea sana kitabu cha Yohane wa Perugia lakini kinatia mkazo zaidi juu ya Fransisko mwenyewe na kuonyesha njia ya kuongoka na kufanana na Kristo ambayo aliifuata na ambayo inawafaa wote.
Kumbe wataalamu wengine leo wanakiona kimeathiriwa na vitabu vya Thoma wa Celano na hata vya Bonaventura wa Bagnoregio juu ya Fransisko, hivyo wanasema kiliandikwa baadaye.
- [1] Archived 20 Novemba 2008 at the Wayback Machine..
- Ngano za Wenzi Watatu – Kumbukumbu ya maisha ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi ilivyoandikwa na Ndugu Leo, Rufino na Angelo – tafsiri ya Ndugu Wafransisko Wakapuchini – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1987
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |