Ngoma Iko Huku ni jina la kutaja albamu yenye nyimbo mchanganyiko kwa vipindi tofauti ya hayati Salum Abdallah akiwa na Cuban Marimba. Albamu imekusanya vibao vyake vyote ambavyo ni vikali na kuviweka pamoja. Hasa kutoka 1955 hadi 1965 mwaka ambao ndio kifo chake kilitokea. Rekodi hizi zilikusanywa na kampuni ya Kijerumani Dizim Records ili kuenzi kazi za mkongwe huyu. Albamu ilitolewa mwaka wa 2000 ikiwa na nyimbo zipatazo 22. Ufundi aliounesha katika nyimbo hizi unapelekea kuonekana kijana hadi sasa. Hata baada ya miaka kupita tangu kufa kwake, lakini bado hata kwa vijana waliozaliwa baadaye wanaelewa mchango wa Salum Abadallah na kuzisikiliza nyimbo zake kwa kiasi kikubwa.[1] Nyimbo nyingi zilikuwa za mapenzi na ukombozi. Hasa kwa vile miaka ile ya 1960 mwanzoni tungo nyingi zilihusu hamasa ya kuileta Afrika huru. Nyimbo kama Beberu na nyimbo zingine za kusifu juhudi za TANU kwa wakati ule.

Ngoma Iko Huku
Ngoma Iko Huku Cover
Greatest hits ya Salum Abdallah na Cuban Marimba
Imetolewa 2000 (miaka ya 1955-1965)
Aina Muziki wa dansi
Lebo Dizim Records

Orodha ya nyimbo

hariri

Hii ni orodha ya nyimbo zilizopo katika albamu hii.

  1. Ngoma Iko Huku
  2. Naumiya
  3. Ubaya
  4. Nalia Nalia
  5. Wanipendeza
  6. Cuba Chacha
  7. Ndiyo Hali Ya Dunia
  8. Kazi Tanzania
  9. Shemeji Shemeji
  10. Tanzania Twist
  11. Sipati Majibu
  12. Salaam Kwa Jumia
  13. Wanawake Tanzania
  14. Kachacha
  15. Tulime Mashamba
  16. Bebru
  17. Kimanzi
  18. Si Kosa Lako
  19. Unavanja Utu
  20. Mpenzi Wee
  21. Maisha Siyatamani
  22. Afrika Muye Muye

Tazama pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri
  1. Salum Abdallah katika DW Swahili. SALUM ABDALLAH ATABAKIA KIJANA MILELE mnamo 28.04.2007