The Tanzania Sound
"The Tanzania Sound " ni jina la kutaja albamu ya nyimbo mchanganyiko ya muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Albamu imekusanya nyimbo za miaka ya 1950-na-1960 na kuziweka pamoja. Albamu ilitolewa tarehe 6 Aprili, 1995. Nyimbo kali kutoka katika albamu ni pamoja na Dada Mwajuma, Tangu Umeondoka, Tukiwa Na Monika Shuleni, Wanawake Tanzania na Shemji Shemeji. Katika miaka ya 1950, Tanzania ilitamba sana kwa muziki wa dansi uliokuwa na hamasa kubwa kushinda hata nchi zake jirani za Zaire na Kenya. Midundo katika kipindi hiki cha miaka ya 1950-1960 ilikuwa balaa.[2]
The Tanzania Sound | ||
---|---|---|
Compilation album ya Mbalimbali | ||
Imetolewa | 6 Aprili, 1995[1] awali ilitoka 1980 na 1993 kisha hii ya 1995 | |
Imerekodiwa | Miaka ya 1950-60 | |
Aina | Muziki wa dansi | |
Urefu | 56:14 | |
Lebo | Original Music |
Orodha ya nyimbo
haririHii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hii.
- A1 – Nimeona Uwa - Kiko Kids
- A2 - Sili, Sishibi, Silali – Kiko Kids
- A3 - Wanawake Wa Tanzania – Salum Abdallah na Cuban Marimba Band
- A4 - Ubeberu – Salim Abdullah na Cuban Marimba Band
- A5 - Vilionitendea – Kilwa Jazz Band
- A6 - Janja Yako – Nuta Jazz Band
- A7 - Mapenzi Tu – Hodi Boys
- A8 - Nora – National Jazz Band
- B1 - Lipa Kodi Ya Nyumba – Western Jazz Band
- B2 - Dunia Ina Mambo – Atomic Jazz Band
- B3 - Fitina Nyingi – Dar Es Salaam Jazz Band
- B4 - Mpenzi Una Nini – Dar Es Salaam Jazz Band
- B5 - Safari Ye Nuta – Nuta Jazz Band
- B6 - Naona Ajabu – Njohole Jazz Band
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ The Tanzania Sound katika wavuti ya Amazon. Audio CD (April 6, 1995).
- ↑ The Tanzania Sound katika All music.com - Tanzania built its own blend of local, Afro-Cuban and Congolese ingredients, and these are its 1950s and 1960s classics. More driving than the Congolese, more dance-oriented than the Kenyans, these Tanzanian bands used local rhythms earlier than most, and also contained some splendid hornmen with very individual sounds. The roots of Mlimani Park, as fresh as on Day One.
Viungo vya Nje
hariri- The Tanzania Sound katika Youtube