Ngome (sataranji)

kete katika mchezo wa sataranji

Ngome (Kiing. rook) ni kete katika mchezo wa sataranji.

Ngome nyeupe
Ngome nyeusi

Kila mchezaji anaanza mchezo na ngome mbili.

Wakati wa kurekodi mchezo ngome inatajwa kwa herufi R.

Mahali pa kuanzia na kusonga

hariri

Mahali pa kuanzia mchezo kwa ngome ni miraba ya A1 na H1 upande mweupe, na A8 na H8 upande mweusi.

Ngome inasonga mbele au nyuma kwenye mistari wima au mlalo kupitia idadi yoyote ya miraba isiyokaliwa na kete nyingine.

Sawa na kete nyingine inanasa kwa kuingia kwenye mraba mwenye kete ya adui.

Ngome na shaha huweza kutekeleza mwendo maalum kama hakuna kete kati yao na zenyewe hazikusogea bado. Hapo ngome inafika kando ya shaha ilhali shaha anaruka juu ya ngome.

Kwa Kiingereza mwendo huo huitwa castling.

 
Mwendo maalum wa ngome na shaha (castling)