Shaha (sataranji)

kete kuu katika mchezo wa sataranji

Shaha ni kete muhimu zaidi katika mchecho wa sataranji. Anaweza kutembea hatua 1 kila upande kwa mraba yoyote jirani. Kifupi chake katika miniti za mchezo ni "K" (kutokana Ing. "king").

Shaha mweupe

Shabaha ya mchezo wa sataranji ni kumkamata shaha. Kwa hiyo ni muhimu kumlinda na kumtetea. Kama shaha anashambuliwa yaani kutishiwa moja kwa moja anapaswa kuondoka katika mraba wake kwenda mraba mwingine asipotishiwa. Kama hakuna mraba bila tishio ameshindwa na mchezo umekwisha.

Mruko mdogo: 0-0
Mruko mkubwa: 0-0-0

Kuruka ngome

hariri

Kuna mwendo 1 wa pekee kama shaha na ngome hazikutembea bado na kete zote zilizopo kati yao zimeshaondoka. Hapa shaha inaruka miraba 2 kuelekea ngome na ngome inaruka upande mwingine wa shaha. Masharti ya mwendo huu ni:

  • wala shaha wala ngome hazikutembea bado
  • hakuna kete tena kati yao
  • shaha haishambuliwi moja kwa moja
  • mraba itakapofikia shaha haitishiwi wakati wa kuruka.

Tishio kwa shaha na kushindwa kwake

hariri

Kama mpinzani anaweza kuitishia kete ya shaha mshambuliwa ana njia tatu:

  • Kuondoka katika mraba unaoshambuliwa kwenda mahali pasiposhambuliwa
  • kukata tishio kwa kuweka kete nyingine kati ya tishio na shaha; hii haiwezekani kama mshambulizi ni kete ya farasi.
  • Kupiga kete inayosababisha tishio

Kama hizi njia 3 zinashindikana upande wa shaha anayetishiwa umeshindwa na mchezo unakwisha.

Mkwamo

hariri

Mkwamo yaani hali ambako hakuna aliyeshinda unatokea kama mchezaji hana nafasi ya kutembea bila kuweka shaha kwenye mraba penye tishio ilhali haikutishiwa bado.

Mchezo

hariri

Wakati wa kuanza machezo wa sataranji na hadi katikati ya mchezo shaha kwa kawaida hatembei isipokuwa kuruka ngome. Mchezaji atalenga kuhifadhi shaha nyuma ya safu ya vitunda.

Lakini katika ngazi za mwishomwisho wa mchezo shaha anakuja mbele mara nyingi akishiriki katika mashambulio na katika mpango wa kubadilisha vitunda kuwa kete za nguvu zaidi.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri

Brace, Edward R. (1977), An illustrated dictionary of chess, Hamlyn Publishing Group, uk. 151, ISBN 1-55521-394-4 Barden, Leonard (1980), Play better chess with Leonard Barden, Octopus Books Limited, ku. 9, 11, 12, ISBN 0-7064-0967-1 Lasker, Emanuel (1934), Lasker's chess primer, Billings (1988 reprint), ISBN 0-7134-6241-8 {{citation}}: More than one of |author= na |last= specified (help)