Niamey ni mji mkuu wa Niger. Iko mwambaoni wa mto Niger. Ikiwa na wakazi 674,950 (sensa ya 2002) Niamey ni mji mkubwa wa Niger na kitovu cha kiutawala, kiuchumi na kiutamaduni.

Jiji la Niamey
Nchi Niger
Niamey wakati wa usiku

Kilimo katika mazingira yya mji kina karanga kama mazao ya sokoni; kuna viwanda vya matofali, saruji na nguo.

Niamey jinsi inavyoonekana kutoka angani

Niamey ilikuwa kijiji kikaanza kukua tangu Ufaransa ulijenga hapa kituo cha kijeshi tangu miaka ya 1890 BK. Mwaka 1926 ikawa mji mkuu wa koloni ya Niger. Mwaka 1930 ilikuwa na wakazi 3,000, wakati wa uhuru mwaka 1960 na wakazi 30,000 na mnamo 1980 na wakazi 250,000.


Viungo vya NjeEdit