Dakar
Dakar ni mji mkuu wa Senegal ikiwa na wakazi 2,352,000. Iko kwenye rasi la Verde ambalo ni pembe la magharibi ya Afrika. Bandari yake ina nafasi nzuri kwa biashara na Ulaya na Amerika.
Jiji la Dakar | |
Nchi | Senegal |
---|
Mji ulianzishwa na Wafaransa mwaka 1857 walipoondoka kisiwa cha Goree kuhamia bara. Ukapata bandari ya biashara na pia bandari ya kijeshi halafu ukawa mwanzo wa reli katika Senegal. Mwaka 1902 Dakar ilikuwa mji mkuu wa Afrika ya Magharibi ya Kifaransa badala ya Saint-Louis. Kati 1959 hadi 1960 ilikuwa mji mkuu wa Shirikisho la Mali, baadaye mji mkuu wa Senegal.
Kisiwa cha Goree ambacho sasa ni sehemu ya mji kilikuwa kati ya vituo muhimu vya biashara ya watumwa. Boma la Fort D'Estrees Gorée kisiwani humo lilikuwa gereza la watumwa kabla ya kupelekwa kwenye meli na leo ni makumbusho.
Walizaliwa Dakar
hariri- Youssou N'Dour, mwimbaji ya mwanamuziki
- Patrick Vieira, mchezaji mpira wa miguu Mfaransa