Nisreen Elsaim

Mwanaharakati kijana wa hali ya hewa kutoka Sudan

Nisreen Elsaim ni mwanaharakati kijana na mzungumzaji wa hali ya hewa kutoka Sudan.[1]

Yuko kwenye Kikundi cha UN cha Vijana cha Ushauri juu ya Mabadiliko ya Tabianchi (UN's Youth Advisory Group on Climate Change) baada ya kuteuliwa na Jumuiya ya Haki ya Hali ya Hewa ya Pan African (Pan African Climate Justice Alliance).[2]

Elsaim ni rais wa Vijana wa Sudan kwa Mabadiliko ya Tabianchi (Sudan Youth for Climate Change).[2] Alikuwa mratibu wa Mkutano wa Vijana wa Hali ya Hewa (Youth Climate Summit) wa 2019.[3]

Elsaim ana shahada ya Fizikia na Nishati mbadala kutoka Chuo Kikuu cha Khartoum.[2][4] Amekuwa akishiriki kikamilifu katika harakati za vijana za hali ya hewa tangu 2012.[5]

Marejeo

hariri
  1. Blazhevska, Vesna. "Young leaders tapped to invigorate UN's climate action plans, hold leaders to account". United Nations Sustainable Development (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-08-27.
  2. 2.0 2.1 2.2 "Sudanese Appointed Chairperson Of UN Advisory Group| Sudanow Magazine". sudanow-magazine.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-19. Iliwekwa mnamo 2020-08-27.
  3. "#YouthParticipation: Nisreen Elsaim, on her journey to becoming a UN Youth Climate". www.fes-connect.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-18. Iliwekwa mnamo 2020-08-27. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. "JWH Initiative". JWHinitiative. Iliwekwa mnamo 2020-08-27.{{cite web}}: CS1 maint: url-status (link)
  5. Blazhevska, Vesna. "Young leaders tapped to invigorate UN's climate action plans, hold leaders to account". United Nations Sustainable Development (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-08-27.