Nishati mbadala ni aina za nishati kutoka vyanzo asilia kama vile mwanga wa jua, nguvu ya upepo, mvua, joto kutoka ardhi, mwendo wa kupwakujaa, kuni au aina nyingine za biomasi na mengine.

Nguvu ya upepo ni chanzo muhimu cha nishati mbadala

Kwa jumla ni vyanzo vya nishati visivyokwisha kutokana na matumizi au kupoa haraka, tofauti na fueli za kisukuku ambazo zinatoka kwenye vyanzo kama makaa mawe, gesi asilia au mafuta ya petroli zinazoendelea kupungua kadiri zinazotumiwa.

Uwekezaji kwenye miradi ya nishati mbadala duniani ulifikia kiasi cha dola za Marekani bilioni 286 mwaka 2015, huku nchi za China na Marekani zikiongoza kwa uwekezaji.[1] Kazi zinazohusiana na nishati mbadala duniani zinakadiriwa kufikia milioni 7.7.[2] Nchi kama Iceland inatumia asilimia 85 ya mahitaji yake ya nishati kutoka nishati mbadala na hivyo kuwa nchi ya kwanza duniani kwa matumizi makubwa ya aina hii ya nishati.[3] Kutokana na ripoti iliyotolewa na REN21 (Renewable Energy Policy Network for the 21st Century', mwaka 2015 nishati mbadala ilichangia asilimia 19.2 ya matumizi ya nishati duniani.[4]

Matumizi ya nishati mbadala

hariri
 
Ufanisi wa vyanzo tofauti vya nishati kwa mwendo wa gari; gari linatumia 11.6 kWh kwa safari lakini kiwango cha nishati asilia inategemea na chanzo na upotevu katika mbinu tofauti za kufukisha nishati hii kwenye mwendo wa gari; mafuta kama chanzo cha nishati huonyesha upotevu mkubwa, yakifuatwa na makaa mawe. Umemejua na umeme upepo ni vyanzo fanisi zaidi zinazopatikana. Picha haionyeshi kiasi cha nishati kinachotumiwa kutengeneza vifaa vya kuzalisha umemejua.

Mwaka 2008 takriban 19-20% ya matumizi ya nishati duniani yametokea kwenye nishati mbadala; wakati ule sehemu kubwa ya takriban asilimia 13 kutoka biomasi hasa kuni na 3.2% kutoka nguvu ya umememaji. [5]

Mwaka 2016/17 kiasi hiki kilibadilika tayari. Biomasi ya kawaida (kuni) ilichangia asilimia 8.9, joto kuoka biomasi, jotoardhi na jotojua 4.2 %, umememaji 3.9 na umemejua pamoja na umeme wa upepo ilikuwa 2.2% . Vyanzo vya kisasa vya nishati mbadala inaogezeka haraka. [6]

Hali halisi manufaa kutoka nishati ya jua ni kubwa zaidi sana kwa sababu matumizi yote ya mimea, mazao na matunda yana nishati ya jua kama msingi wake; pia kiwango cha joto la mazingira kinasababishwa na jua lakini katika takwimu hizi zinataja viwango tu vinavotumiwa na jitihada za binadamu kubadilisha mazingira asilia kama kupasha moto nyumbani, kupika vyakula, uzalishaji umeme, kuendesha usafiri na kadhalika.

Katika uzalishaji wa umeme duniani asilimia ya nguvu ya umememaji ilikuwa takriban 15%.

Kuongezeka kwa nguvu ya upepo

hariri

Teknolojia ya kuzalisha umeme wa upepo imepanuka sana katika miaka iliyopita. Mwisho wa mwaka 2009 ujazifu wa umeme kutoka chanzo hiki ulikuwa megawati 157,900 ambazo ni ongezeko la 31% tangu mwanzo wa mwaka uleule. [7]

Maendeleo hayo mwanzoni yalitokea Ulaya, hasa Ujerumani, Udani na Uingereza lakini baadaye Marekani na China ziliongeza pia jitihada zao kupanua chanzo hicho cha umeme. [8][9]

Katika nchi ya Denmark umeme kutoka nguvu ya upepo ni tayari asilimia 19 ya matumizi yote ya kitaifa. [10]

 
Nellis Solar Power Plant inazalisha umemenuru kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani.

Seli za umemejua zinabadilisha mwanga wa jua kuwa umeme. Teknolojia hiyo inaendelea haraka sana na gharama za seli hizi zinashuka. Kuna vituo vingi, hasa Ulaya, ambako serikali zimetoa misaada kwa ajili ya kutegeneza vituo hivyo na matumizi ya teknolojia hiyo. [11]

Mwisho wa mwaka 2010 vituo vikubwa duniani vilikuwa :

Vituo vikubwa zaidi hutengenezwa.[12]

Marejeo

hariri
  1. REN21, Global Status Report 2016. Retrieved 8th June 2016.
  2. IRENA, Renewable energy and jobs, Annual review 2015, IRENA.
  3. Iceland Energy Portal.
  4. REN21 Ilihifadhiwa 27 Julai 2018 kwenye Wayback Machine..
  5. REN21 (2010). Renewables 2010 Global Status Report Ilihifadhiwa 16 Aprili 2012 kwenye Wayback Machine. p. 15-16.
  6. [www.ren21.net/wp-content/uploads/2016/06/GSR_2016_FullReport_.pdf Taarifa ya Ren21 kwa 2016]
  7. Lars Kroldrup. Gains in Global Wind Capacity Reported Green Inc., 15 Februari 2010.
  8. Global wind energy markets continue to boom – 2006 another record year Ilihifadhiwa 7 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine. (PDF).
  9. Global Wind Energy Council (2009). Global Wind 2008 Report Ilihifadhiwa 7 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine., p. 9, accessed on 4 Januari 2010.
  10. International Energy Agency (2009). IEA Wind Energy: Annual Report 2008 Ilihifadhiwa 29 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine. p. 9.
  11. Denis Lenardic. Large-scale photovoltaic power plants ranking 1 - 50 PVresources.com, 2010.
  12. Mark Z. Jacobson (2009). Review of Solutions to Global Warming, Air Pollution, and Energy Security Ilihifadhiwa 2 Juni 2010 kwenye Wayback Machine. p. 4.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nishati mbadala kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.