Nkem Owoh
Nkem Owoh ni muigizaji na mchekeshaji wa Nigeria. Mwaka 2008 alishinda tuzo ya African Movie Academy Award kama Muigizaji Bora katika sehemu ya uongozi. [1]
Nkem Owoh | |
---|---|
Amezaliwa | Nkem Owoh Enugu Nigeria |
Kazi yake | Muigizaji |
Maisha Yake ya Utotoni
haririOwoh alizaliwa Enugu Nigeria Baada ya masomo yake ya msingi na ya upili, alienda Chuo Kikuu cha Ilorin alikosomea uhandisi. Kama bado anasoma masomo ya chuo kikuu, Owoh alianza uigizaji katika televisheni na filamu.
Kazi
haririOwoh alikuwa kati ya waigizaji wakuu katika filamu ya 2003 ya Osuofia i London . Anajulikana pia kwa kuuimba wimbo wa I Go Chop Your Dollar, unaohusu ufisadi wa ada ya mapema. Wimbo huu ulitumika katika filamu ya The Master ambapo Owoh hucheza kama mtapeli.[2] Tume ya Uhalifu wa Fedha na Uchumi na Tume ya Utangazaji ya Nigeria ilipiga marufuku wimbo huo[3]. Mwaka 2007 alikamatwa na polisi mjini Amsterdam, Uholanzi(kitongoji Bijlmermeer katika eneo la Amsterdam Zuidoost) kama matokeo ya uchunguzi wa miezi 7 ulioitwa "Operation Apollo".[2] Owoh alikuwa akitumbuiza wakati polisi walivamia pahali pale na kuwatia mbaroni watu 111 kwa tuhuma za udanganyifu makosa ya uhamiaji. Owoh baadaye aliachiliwa huru.[3][4][5] Mwezi Novemba 2009, Owoh alitekwa nyara eneo la mashariki mwa Nigera. Wateka nyara walitaka naira milioni 15 kama makombozi. Aliachiliwa huru baada ya familia yake kutoa naira milioni 1.4 kama makombozi.
Filamu
haririMwaka | Filamu | Jukumu | Vidokezo |
---|---|---|---|
1987 | Things fall apart | na Pete Edochie | |
1995 | Ukwa | na Patience Ozokwor | |
1999 | Big Man...Big Trouble | ||
Conspiracy | na Onyeka Onwenu | ||
2001 | Onye-Eze | Onye-Eze | |
2002 | Fake Doctor | Dr. Zebedi | |
Ifeonye metalu | |||
Long John | |||
Police Officer | |||
Spanner | na Chinedu Ikedieze | ||
2003 | Anunuebe | ||
King of the Forest | |||
Lion Finger | |||
Mr. Trouble | na Patience Ozokwor | ||
Osuofia in London | |||
Police Recruit | |||
2004 | America Visa | ||
My Driver | |||
My Own Share | |||
Osuofia in London 2 | |||
Spanner Goes to Jail | na Chinedu Ikedieze | ||
2005 | Akanchawa | ||
Bus Driver | na Dakore Egbuson | ||
The Prince | |||
2006 | A Fool at 40 | Hygenius | |
Captain | |||
Foreign Base | |||
Indemnity | Egbentu | ||
Made in Cambridge | |||
My Kingdom Come | |||
The Barrister | Athanasius | ||
The Dreamer | |||
2007 | Battle of Indemnity | Egbentu | |
Covenant Keeping God | Samuel | ||
De prof | |||
Johnbull & Rosekate | Johnbull | ||
Persecution | |||
Stronger Than Pain | Ulonna | na Kate Henshaw-Nuttal Uigizaji wake katika filamu hii ulifanya apewe tuzo la Best Actor in a Leading Role katika African Movie Academy Awards mwaka 2008 | |
2008 | His Holiness | ||
His Last Action | |||
Wonderful Man |
Marejeo
hariri- ↑ "AMAA 2008: List of Winners". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-26. Iliwekwa mnamo 2009-11-11.
- ↑ 2.0 2.1 Jan Libbenga (2007-07-02). "'I Go Chop Your Dollar' star arrested". The Register.
- ↑ 3.0 3.1 "Police Arrest Nkem Owoh in Holland". NigeriaMovies.net. 2007-07-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2009-12-23.
- ↑ "'I Go Chop Your Dollar' star arrested". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-16. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2009.
- ↑ | Jan Libbenga (2021-03-30). I Go Chop Your Dollar star arrested
Viungo vya nje
hariri- Nkem Owoh at the Internet Movie Database