Northumberland ni kaunti ya Uingereza iliyopo kwenye mpaka wa Uskoti. Jina limetokana na mahali pake upande wa kaskazini wa mto Humber. Ni sehemu ya mkoa wa Uingereza Kaskazini-Mashariki.

Eneo la Northumberland

Ina eneo la km² 5,013 na idadi ya wakazi ni 316.116[1]. Makao makuu ya mkoa yapo kwenye mji mdogo wa Morpeth mwenye wakazi 13,833. Ngome ya Chillingham Castle iko hapa.

Marejeo hariri

  1. Sensa 2011, kupitia archive.org