Nota nzima (muziki)

Nota nzima (kwa Kiingereza: Whole note au semibreve) ni aina ya nota za muziki itumikayo katika uandishi wa muziki na ina thamani ya mapigo manne (4). Nota nzima huwa na umbo la sifuri au 0 kama ionekanavyo katika picha.

Nota nzima na pumziko lake.

Pumziko la nota nzima

hariri

Pumziko la Nota nzima huwa na umbo la kisanduku kilichotiwa kivuli na kutazamia chini, na huchorwa katika mstari mmojawapo kati ya mistari mitano ya staff ya muziki. Pumziko la nota nzima huwa na thamani ya mapigo manne (4), yaani thamani ya mapigo yake ya ukimya hufanana na thamani ya mapigo ya nota nzima. [1]

Marejeo

hariri
  1. Morehen, John, and Richard Rastall. 2001. "Semibreve". The New Grove Dictionary of Music and Musicians, second edition, edited by Stanley Sadie and John Tyrrell. London: Macmillan Publishers.