Nusutufe ya kusini

Nusutufe ya Kusini: Antaktika (katikati), Amerika Kusini (juu kushoto), Afrika (juu kulia), Australia na eneo la Pasifiki
Tofauti ya viwango vya bahari na nchi kavu kati ya nusutufe za dunia

Nusutufe ya kusini (en:Southern Hemisphere) ni nusu ya Dunia ilioko upande wa kusini ya ikweta.

Tofauti na nusutufe ya kaskazini hii kusini ya Dunia ina maeneo makubwa zaidi ya bahari ambayo ni asilimia 80.9%, ilhali kwenye kaskazii ni asilimia 60.7% pekee. Theluthi moja yaani 32.7% za nchi kavu ya Dunia iko kwenye nusutufe ya kusini.[1]

Kati ya mabara ni yote ya Antaktiki na Australia, asilimia 90 za Amerika Kusini na theluthi ya kusini ya Afrika yaliyopo kwenye nusutufe. Kuna pia visiwa vikubwa vya Asia zilizopo kusini ya ikweta na visiwa vingi nya Pasifiki. [2]

Majira ya joto huwa ni hapa kuanzia Disemba hadi Machi, na majira baridi kuanzia Juni hadi Septemba.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  1. (2002) Life on Earth: A - G.. 1. ABC-CLIO, 528. ISBN 9781576072868. Retrieved on 8 September 2016. 
  2. (2002) Life on Earth: A - G.. 1. ABC-CLIO, 528. ISBN 9781576072868. Retrieved on 8 September 2016.