Nyenje-ardhi kibete

Nyenje-ardhi kibete
Jike la Nemobius sylvestris
Jike la Nemobius sylvestris
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Ensifera (Wadudu kama nyenje)
Familia ya juu: Grylloidea (Nyenje)
Laicharting, 1781
Familia: Trigonidiidae
Saussure, 1874
Nusufamilia: Nemobiinae
Saussure, 1877
Ngazi za chini

Kabila 6:

Nyenje-ardhi vibete (kutoka kwa King. pygmy field cricket) ni wadudu wa nusufamilia Nemobiinae katika familia Trigonidiidae ya oda Orthoptera wanaofanana na nyenje-ardhi wadogo. Majike wana oviposito nyofu (neli ya kutagia mayai).

Maelezo

hariri

Nyenje hawa ni wadogo kiasi wenye urefu wa mm 7 hadi 15 na upana wa mwili kwa ujumla si zaidi ya mm 3. Mwili wote una nywele nyingi na haswa sehemu ya juu ya kichwa na pronoto; zile za pronoto ni ndefu kiasi. Mabawa yana urefu wa kawaida au ni mafupi au hayawepo. Tibia hubeba miiba. Serki ni ndefu kiasi. Majike wana oviposito ndefu na nyofu na siyo bapa[1].

Madume wenye mabawa kwa kawaida huimba au hutoa nyende (stridulation) kwa kusugua mabawa za mbele kupitia stridulo. Mwisho huo una "kioo" kidogo tu, eneo lisilo na vena[1].

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Gabusibius litoreus
  • Pteronemobius chopardi
  • Pteronemobius heydenii
  • Pteronemobius niveipalpus
  • Pteronemobius pseudotaprobanensis
  • Pteronemobius quadrilineatus
  • Pteronemobius troitzkyi
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyenje-ardhi kibete kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. 1.0 1.1 Desutter-Grandcolas et al. (2021) Updated diagnoses for the cricket family Trigonidiidae (Insecta: Orthoptera: Grylloidea) and its subfamilies (Trigonidiinae, Nemobiinae), with a review of the fossil record. Zoologischer Anzeiger 294: 80-91.