Nyenje mkia-kitara
Nyenje mkia-upanga | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Trigonidium sp.
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Kabila 2:
|
Nyenje mkia-kitara (kutoka kwa King. sword-tail cricket) ni wadudu wa nusufamilia Triogonidiinae katika familia Trigonidiidae ya oda Orthoptera wanaofanana na nyenje-ardhi wadogo. Majike wana oviposito (neli ya kutagia mayai) kwa umbo la kitara na siyo upanga, kama jina la Kiingereza linavyodokeza.
Maelezo
haririNyenje hawa ni wadogo hadi wadogo sana wakiwa na urefu wa mwili wa mm 4 hadi 15 na upana wa mwili kwa ujumla si zaidi ya mm 3. Mwili wote una nywele nyingi na haswa sehemu ya juu ya kichwa na pronoto. Wana kichwa kidogo cha pembetatu na macho makubwa ikilinganishwa na ukubwa wao, ambayo kwa kawaida hujitokeza kwa mtazamo kutoka juu. Pronoto ni nyembamba kuliko kichwa. Tibia hubeba miiba. Majike wana oviposito ndefu kiasi kwa umbo la kitara. Viungo vya uzazi vya kiume ni vidogo sana na bapa na vimerefuka[1].
Kwa kawaida madume huimba au kutoa nyende (stridulation} kwa kusugua mabawa ya mbele kupitia stridulo. Mwisho huo una "kioo" kilichoendelezwa vizuri, eneo lisilo na vena.[1].
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri- Anacyrtoxipha albotibialis
- Anaxipha kilimandjarica
- Anaxipha sjostedti
- Anaxipha vadschaggae
- Metioche massaica
Picha
hariri-
Anaxipha exigua
-
Metioche maorica
-
Metioche sp.
-
Trigonidium cicindeloides
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyenje mkia-kitara kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |