Nyoka-chale
Nyoka-chale | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyoka-chale Madoadoa (Homoroselaps lacteus)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 2:
|
Nyoka-chale ni nyoka wenye sumu wa jenasi Homoroselaps katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu ya milia yao ya rangi nzuri. Wanatokea Afrika ya Kusini.
Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 65 kwa kipeo lakini sm 20-40 kwa kawaida. Wana mlia njano au mwekundu kwa urefu mzima wa mgongo na milia myeusi au mabaka meusi mbavuni.
Nyoka-chale hupumzika katika vichuguu na kuwinda kati ya manyasi na katika takataka za majani ambapo hukamata mijusi (mijusi bila miguu hasa) na nyoka wengine wadogo kama birisi.
Chonge ni meno ya nyuma. Nyoka hawa wanaweza kung'ata lakini sumu siyo hatari sana. Hata hivyo inaweza kusababisha kufura na maumivu makali ya kichwa.
Spishi
hariri- Homoroselaps dorsalis, Nyoka-chale Milia (Striped harlequin snake)
- Homoroselaps lacteus, Nyoka-chale Madoadoa (Spotted harlequin snake)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-chale kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |