Vertebrata
Mjusi ni mfano wa vertebrata
Mjusi ni mfano wa vertebrata
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Chordata
Nusufaila: Vertebrata
Cuvier, 1812
Ngazi za chini

Ngeli 9 (uainisho wa kimila):

Vertebrata ni jina la kitaalamu la kutaja wanyama wote wenye uti wa mgongo. Mifano ni mamalia, ndege (Aves), reptilia (wanyama watambaaji kama nyoka au mamba) na samaki. Mwanadamu pia huhesabiwa humo kibiolojia.

Mbwa ni mfano wa wanyama wa vertebrata

Vertebrata wana kiunzi cha ndani, neva kuu zinapitishwa ndani ya uti wa mgongo zinapohifadhiwa ndani ya ganda la mfupa. Kuna kitovu cha neva upande wa juu ya uti wa mgongo na kwa wanyama walioendelea zaidi kitovu hiki kimeendelea kuwa ubongo unahifadhiwa ndani ya fuvu.

Vertebrata wako kote duniani kwenye mabara yote na aina mbalimbali za mazingira kuanzia nchi kavu, baharini hadi tako la bahari na hewani (ndege). Takriban spishi 58.000 zinajulikana. Ni wanyama wakubwa maana wanyama wasio na uti wa mgongo kwa jumla ni wadogo zaidi hadi wadogo sana.

Uainisho

hariri


Viungo vya Nje

hariri