Nyotamwako
Nyotamwako (kwa Kiingereza: Blazar) ni kiini cha majarra hai kinacho mchirizi husianifu (mchirizi mwenye maada ya ioni unaoenda kwa karibu na kasi ya nuru) kuelekea kwa mtazamaji. Ukuzaji husanifu wa mnururisho sumakuumeme kutoka mchirizi huongeza mng'aro wa nyotamwako. Nyotamwako ni vyanzo vyenye nguvu sana vya mnururisho pote pa taswirangi sumakuumeme na hutoa fotoni za miali-X yenye nishati ya juu. Nyotamwako ni badilifu mno; kwa kawaida mng'aro wake hubadilika sana katika muda mfupi (saa hadi siku).
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyotamwako kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |