Ondoa Giza Kitaa
"Ondoa Giza Kitaa" ni wimbo uliotoka tarehe 21 Februari, 2017 kutoka kwa msanii mzuki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Sir Elly Mandella akiwa na Nari MC na Prime Number. Wimbo umetayarishwa na Man DVD kupitia studio za Bokazy Entertainment. Wimbo unatoka katika albamu ya M99 the Root. Awali ulitambulishwa mnamo Februari 16 2017 ukiwa kama audio na kutolewa rasmi wiki moja baadaye. Ndani ya wimbo wanazungumzia mabaya yanayoendelea mtaani na kuyataka yakomeshwe kwa mikono yetu wenyewe. Wimbo umezungumzia umalaya, mimba za utotoni, madawa ya kulevya, unafiki na maisha halisi ya mtaani.
"Ondoa Giza Kitaa" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Sir Elly akiwa na Nari MC na Prime Number
kutoka katika albamu ya M99 the Root | ||
Umetolewa | 21 Februari, 2017 | |
Umerekodiwa | 2017 | |
Aina ya wimbo | Hip hop | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 4 | |
Studio | Bokazy Entertainment | |
Mtunzi | Sir Elly Nari Mc Prime Number | |
Mtayarishaji | DVD Man |
Maudhui
haririUbeti wa kwanza Sir Elly;
Mwanzo tu mshangao wa baba kumkataa mtoto wake. Ugumu wa maisha uliopelekea dada zete kujiuza. Ukiangalia kwa kina Sir Elly anaona ugumu wa maisha sio kisingizio cha kufanya uhasherati kwa kujipatia kipato. Wangapi hawafanyi hayo na maisha yanaenda. Dhahiri kiza kimetanda ndio maana anasema ondoa giza kitaa. Wapo wengine wanaojita mambo safi mtaani na kunata, punde wanashika mimba na nyodo zote zinaisha. Kwa aibu anaamua kuwa kimya na limimba lake alilotoswa. Mimba za utotoni zinazungumzwa humu, jambo la kusikitisha kuona jamii inayotuzunguka inatazama jinsi wasichana wadogo wanavyodhalilishwa kwa kuzaa katika umri mdogo. Uzazi wa umri mdogo unachangamoto nyingi sana. Lakini juhudi za dhati hazijafanyika. Sir Elly anaona hili ni jukumu la kila mwanajamii kusimamia watoto wetu mtaani. Mtoto wa mwenzako ndio wako. Anaona siku hizi watoto wadogo si wadogo tena. Watoto wadogo wana mambo ya kikubwa hakuna mfano. Mtoto mdogo ana maovu rundo. Unatumwa ujumbe uwafikie watu wote wanaojiona wakubwa kuliko wenzao. Suala la kuuza ngada linaendelea kama kawaida, japo kunaonekana juhudi za kisiasa katika kusimamia suala hili. Huduma bado inapatikana licha ya mikwara mingi kuchimbwa. Sir Elly anaona ukiwachana kwa njia ya sanaa itasaidia kueneza habari za ukatazo dhidi ya usambazaji wa dawa za kulevya. Halafu Sir Elly anaitikia kwa kusema:
"Mbele giza, Nyuma giza"
"Nje giza, ndani giza"
"Sijui hata wapi pa kuelekea, maana kote mimi ninaona giza aah"
"Ondoa giza, ondoa giza, ondoa giza kitaaa aah"
Ubeti wa Nari MC
haririNari anaona watu wana mawazo ya kijinga kiasi kwamba hata lililo mbele yao wanashindwa kuliona. Anarejea maneno ya "Macho Ngumu Kuona". Uwoga katika maisha haukufanyi kufanikiwa bali kukudumaza. Sio kwamba ukiwa muoga ndio utaenda peponi. Namna ya ufundishaji ambao sio rafiki kwa wasomeshwaji. Watu hawaelewi kitu. Bado kuna wengine wanajifanya watumikia hip hop kumbe ndio wanafiki wakubwa katika suala zima la kuiponda. Wanashangazwa pamoja na majungu yao ndio kwanza muziki unapaa. Wanabaki na maswali tu. Vilevile anarejea jinsi Kilimo Kwanza kilivyoshindwa kumsaidia mtu wa hali ya chini. Nari anachukizwa na marafiki bandia wanajiofanya wanaeneza upendo ilhali wanaeneza skendo.
Ubeti wa Prime Number
haririPrime anaona ukubwani hakuna rafiki wa kudumu, na mwisho wa siku kila mtu lazima arudi kwa Mola wake. Maisha ni kupanda na kushuka, kufanikiwa au kutofanikiwa. Lakini mafanikio yako isiwe sababu ya wewe kujifanya hunijui au kunikana. Mwisho wa siku sote njia yetu ni moja. Tuishi kwa upendo. Prime anaona ulimwengu umebadilika sana. Mambo machafu yamekuwa kawaida katika jamii iliyotuzunguka. Wizi, ulaghai utapeli na kadhalika. Ubinadamu umepungua kiasi kwamba hata unasikia mlio wa bunduki hushituki tena. Unaona kawaida hata kama kuna mtu kauawa katika mlio huo. Anasikitishwa namna watu wanavyopandikiziana chuki kwa manufaa binafsi. Analitoa la moyoni kila mja alisikie. Anato fumbuzi kwa wale wenye vijiba vya nafsi kwa wenzao. Anatumia misamiati ya kuficha maneno makali katika sanaa. Jinsi wakubwa wanavyoonea wadogo kwa kutumia nyadhifa zao. Walio juu kuwaona walio chini hawana akili. Rejea mstari kama:
"Kinywa cha kibogoyo ikiweka mfupa ni mateso",
"Naona nguvu kwenye maji ndani ya mawe",
"Nguvu ya mtu kwa mtu na mwanawe"
Tazama pia
haririViungo vya Nje
hariri- Video ya Ondoa Giza Kitaa katika YouTube
- Ondoa Giza Kitaa katika wavuti ya Mdundo