One Billion Rising
One Billion Rising ni kampeni ya kimataifa, iliyoanzishwa na Eve Ensler kukomesha ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Ilianzishwa mnamo mwaka 2012 kama sehemu ya harakati ya V-Day. "Bilioni" inahusu takwimu za Umoja wa Mataifa kwamba mwanamke mmoja kati ya watatu huwa anabakwa au kupigwa katika maisha yake.
Kuanzishwa
haririKampeni hiyo ilianzishwa na mwandishi wa tamthilia na mwanaharakati Eve Ensler (anayejulikana kwa tamthilia yake ya The Vagina Monologues), na shirika lake la V-Day.