Ubakaji (kutoka mzizi wa Kiarabu) ni tendo la kumlazimisha mtu afanyiwe asichokubali. Mara nyingi neno hili linatumika kuhusu ngono isiyo ya hiari upande mmojawapo.

Ubakaji wa Lukresya, uliomfanya ajiue, ulikuwa kati ya sababu za mfululizo wa matukio yaliyokomesha Ufalme wa Roma na kuanzisha Jamhuri ya Roma mwishoni mwa karne ya 6 KK.
Maandamano huko Bangalore, India, yakidai haki kwa mwanafunzi aliyebakwa huko Delhi mwaka 2012. Ubakaji nchini huko unaongezeka kwa kasi kutokana na dharau kwa wanawake.

Ingawa kwa kawaida unafanyika dhidi ya wanawake, unatokea pia dhidi ya wanaume, mbali ya watoto na walemavu wa akili wasioelewa kinachoendelea[1].

Unaweza kutumia nguvu ya mwili, lakini pia mamlaka, vitisho n.k.

Ni tukio baya kabisa kwa nafsi ya mhanga na pengine kwa afya yake, linaloweza kumuathiri maisha yake yote kama si kusababisha kifo chake, hasa ukifanywa na watu kadhaa pamoja.

Matukio ya namna hiyo yanazidi kutokea hata ndani ya ukoo na mengi hayaripotiwi kwa polisi, yakiwemo yanayotokea magerezani kati ya watu wa jinsia ileile.

Kwa vyovyote, mara nyingi wanaobaka ni watu wanaojulikana sana na mhanga.

Pengine ubakaji hautokani na tamaa, bali ni mpango uliosukwa na viongozi wa nchi au wa jeshi wanaouagiza kwa lengo la kuathiri maadui. Lakini hata vitani, sheria za kimataifa haziruhusu matendo hayo ya kinyama.

Kesi tofauti tena ni ile ya ushirikina unaoagiza k.mf. kubaka mtoto kama njia ya kupona UKIMWI.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubakaji kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.