Otago Daily Times
Otago Daily Times (ODT) ni gazeti la kila siku linalochapishwa na kampuni ya Allied Press katika eneo la Dunedin, New Zealand.
Otago Daily Times | |
---|---|
Jina la gazeti | Otago Daily Times |
Aina ya gazeti | Gazeti la kila siku isipokuwa Jumapili |
Lilianzishwa | 1861 |
Nchi | New Zealand |
Mhariri | Murray Kirkness |
Mmiliki | Allied Press |
Mchapishaji | Allied Press |
Makao Makuu ya kampuni | Dunedin |
Nakala zinazosambazwa | 43,000 |
Tovuti | http://www.odt.co.nz/ |
Historia
haririGazeti la ODT lilianza kuchapishwa mnamo tarehe 15 Novemba 1861. Hili ndilo gazeti kongwe kabisa la kuchapishwa kila siku nchini New Zealand. Gazeti jingine kongwe ni la Christchurch , The Press, ambalo ni kongwe kuliko ODT kwa miezi sita , lilikuwa gazeti la kuchapishwa kila wiki katika miaka yake ya kwanza lakini likabadilika na kuwa la kila siku.(Hivyo basi ODT ndilo kongwe katika sekta ya magazeti ya kila siku.)
Gazeti la ODT lilianzishwa na W.H. Cutten na Julius Vogel (hapo baadaye aliitwa Sir Julius) katika nyakati za uchimbuzi wa dhahabu katika eneo lao la Tuapeka, mojawapo ya maeneo ya Otago yaliyopatikana kuwa na dhahabu. Cutten alikuwa mchapishaji wa gazeti la kila wiki la the Otago Witness lililoanzishwa katika mwaka wa 1851. Vogel naye , mwanzilishi mwenzake Cutten, aliliona gazeti hili la ODT kama mbinu ya kutetea na kupinga sera mbalimbali katika serikali ya mikoa.
Kutoka kuanzishwa kwake, ODT lilikuwa na msimamo dhabiti katika soko la magazeti katika eneo la South Island. Magazeti mengine pinzani ya Dunedin yalikwisha haraka(labda kwa kushindwa na ODT huku gazeti la Evening Star pekee yake likiweza kufika miaka ya 1900. Wamiliki wa Star walinunua gazeti la ODT na kuachisha uchapishaji wa Star katika mwaka wa 1978 kwa sababu idadi ya wasomaji ilikuwa ikididimia.Kama matokeo ya hayo, kampuni ya Allied Press inachapisha ODT na magazeti mengine madogo kote nchini New Zealand, kwa mfano: Greymouth Evening Star.
Gazeti la ODT huonekana kama gazeti baba kwa magazeti mengine manne makuu ya kila siku ya New Zealand. Gazeti hili lina usambazaji wa nakala 43,000 na wasomaji takriban 110,000.
Sera zake
haririKatika miaka yake ya mwanzo, ODT lilihusika katika kampeni nyingi za kupigania haki za jamii. Mfano mmoja ni liliporipoti kuhusu mazingira mbovu ya kazi katika eneo la Dunedin ,katika miaka ya 1880. Ripoti hizi ,zilizoandikwa chini ya Mhariri Sir George Fenwick na Mwandishi Mkuu Silas Spragg, zilisababisha mageuzi makubwa ya kisheria.
Sid Scales alikuwa mchoraji wa katuni wa gazeti la ODT kwa miaka 30 mpaka alipostaafu katika mwaka wa 1981. Tangu mwaka huo, mchoraji Garrick Tremain akawa mchoraji mkuu wa katuni wa gazeti hilo. Mhariri wa gazeti ni Murray Kirkness, aliyechukua hadhi hii kutoka mhariri wa muda mrefu, Robin Charteris mnamo Aprili 2007.
Marejeo
hariri- Reed, A.H. (1956) The story of Early Dunedin. Dunedin: A.H. & A.W. Reed.
- The Otago Daily Times Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
hariri- Otago Daily Times tovuti rasmi ya gazeti hili
- Allied Press tovuti rasmi ya wachapishaji
- National Library of New Zealand Online Newspaper Archive