Kuzumburu

(Elekezwa kutoka Pasa)
Kuzumburu
Kuzumburu michirizi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Coliiformes (Ndege kama kuzumburu)
Familia: Coliidae (Ndege walio na mnasaba na kuzumburu)
Swainson, 1837
Ngazi za chini

Jenasi 2 na spishi 6:

Kuzumburu au pasa ni ndege wa familia Coliidae. Spishi zote zinatokea Afrika chini ya Sahara. Ndege hawa ni wadogo kadiri na wana mkia mrefu na kishungi kichwani. Rangi yao ni kijivu au kahawia. Huenda kwa makundi matawini kwa miti wakitafuta majani, maua na matunda ya kulika. Mwenendo huu unafanana ule wa panya na kwa sababu hiyo waitwa “mousebirds” (ndege-panya) kwa Kiingereza na majina yanayofanana kwa lugha nyingine. Kuzumburu hujenga matago kwa vitawi yenye umbo wa kikombe ambayo yamefunikwa ndani kwa manyasi. Jike huyataga mayai 2-4 na kinda huondoka tago baada ya muda mfupi tu.

Spishi

hariri