Kuzumburu
(Elekezwa kutoka Urocolius)
Kuzumburu | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 2 na spishi 6:
|
Kuzumburu au pasa ni ndege wa familia Coliidae. Spishi zote zinatokea Afrika chini ya Sahara. Ndege hawa ni wadogo kadiri na wana mkia mrefu na kishungi kichwani. Rangi yao ni kijivu au kahawia. Huenda kwa makundi matawini kwa miti wakitafuta majani, maua na matunda ya kulika. Mwenendo huu unafanana ule wa panya na kwa sababu hiyo waitwa “mousebirds” (ndege-panya) kwa Kiingereza na majina yanayofanana kwa lugha nyingine. Kuzumburu hujenga matago kwa vitawi yenye umbo wa kikombe ambayo yamefunikwa ndani kwa manyasi. Jike huyataga mayai 2-4 na kinda huondoka tago baada ya muda mfupi tu.
Spishi
hariri- Colius castanotus, Kuzumburu Mgongo-mwekundu (Red-backed Mousebird)
- Colius colius, Kuzumburu Mgongo-mweupe (White-backed Mousebird)
- Colius leucocephalus, Kuzumburu Kichwa-cheupe (White-headed Mousebird)
- Colius striatus, Kuzumburu Michirizi (Speckled Mousebird)
- Urocolius indicus, Kuzumburu Uso-mwekundu (Red-faced Mousebird)
- Urocolius macrourus, Kuzumburu Kisogo-buluu (Blue-naped Mousebird)
Picha
hariri-
Kuzumburu mgongo-mweupe
-
Kuzumburu kichwa-cheupe
-
Kuzumburu uso-mwekundu
-
Kuzumburu kisogo-buluu