Pathfinder ni filamu ya mapigano ya mwaka wa 2006 iliyoongozwa na Marcus Nispel. Ndani yake anakuja Karl Urban na Moon Bloodgood wakiwa kama vinara wa filamu hii. Ilitolewa mnamo tar. 13 Aprili 2006 na toleo la DVD lilitolewa mnamo 31 Julai 2007. Ilipewa hadhi ya R nae MPAA kwa nguvu na mauaji ya kikatili yanayofanywa kwenye filamu. Hadithi ya filamu inaeelezea uvamizi haramau wa Waviking na wenyeji halisi wa Marekani.

Pathfinder
Imeongozwa na Marcus Nispel
Imetayarishwa na Marcus Nispel
Mike Medavoy
Arnold W. Messer
Imetungwa na Laeta Kalogridis
Nyota Karl Urban
Moon Bloodgood
Russell Means
Imehaririwa na Jay Friedkin
Glen Scantlebury
Imesambazwa na 20th Century Fox
Imetolewa tar. 13 Aprili 2006
Ina muda wa dk. 99 mins.
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza, Kiicelandi
Bajeti ya filamu $31 milioni[1]

Washiriki

hariri
  • Karl Urban - Ghost
  • Moon Bloodgood - Starfire
  • Russell Means - Pathfinder
  • Jay Tavare - Blackwing
  • Clancy Brown - Gunnar
  • Ralf Moeller - Ulfar

Muhtsarai wa hadithi

hariri

Kijana ambaye atakayekuja kuitwa Ghost alikuwa na kundi la wakoloni la Waviking ambao wamekusidia kuondoasha idadi ya wenyeji. Wakati picha inaanza inaonekana mabaki ya boti refu ambalo linamilikiwa na hao majitu, ndani yake wamemwacha Ghost akiwa kama nafsi iliyosalia ikiwa hoi bin taabani. Mwanamke mmoja ambaye ni mwenyeji wa pale aliingia ndani ya boti lile na kumkuta Ghost akiwa ndani na kumchukua na kwenda kumlea akiwa kama mwanae wa kumzaa.

Miaka kadhaa baadaye, Ghost akiwa bado anasumbuliwa na ndoto zake, ambapo ikiambatana pamoja na tofauti ya mwonekano wake, imeingiliana na uwezo na kuweza kuwa kama mmoja wa wanajumuia ile. Yeye anahisia za kimapenzi na mwanama mmoja kutoka katika kabira hilo ambaye aliitwa Starfire, binti wa Pathfinder, mtu anayemtafuta mrithi atakayefaa katika Uhalifa.

Baadaye, wakati anawinda huku wakiwa wametawanyika kwa makundi, msichana mdogo kutoka katika kabira la Ghost akaenda mbali na eneo ambalo hakutakiwa aende, akavamiwa na vijana wa Waviking na kumshambulia. Kwa bahati akaweza kutoroka na kurudi kule kijijini kwao, lakini alifuatwa na Waviking. Wameangamiza kijiji na kuchinja karibuni kila mtu aliyopo kijiji hapo, ila watu wachache ambao wanataka kuwaua mmoja mmoja katika "mashindano ya kupigana".

Ghost akarejea pale kijijini, lakini akawa kachelewa kufika pale hivyo kashindwa kuwasaidia wanakijiji wale na kumkuta mama yake mlezi akiwa kauawa na Gunnar, kiongozi wa Waviking. Haikuishia hapo, Waviking wakamtaka Ghost wapigane mtu mbili; akamtofoa mpinzani wake na kukimbia katika eneo lile. Akiwa mbioni, akaumizwa, akiwa mbioni akapata kujificha katika pango ambapo baadaye alikuja kukutwa na lile kabila ambalo walitawanyika pale awali ili kwenda kuwinda.

Wakamrudisha nyumbani, na mashujaa wa pale wakasuka mpango dhidi ya wavamizi wao Waviking. Ghost, lakini, alieleza unyama na ukatili wa maadui zao, na kuwaonya kwamba silaha zao za miti na mawe hazifui dafu kwa silaha za machuma na mapanga ya Waviking. Ghost aliwashauri wanakijiji hao kwamba nafasi yao ya kuponyeka ni kukimbia kutoka katika eneo hilo na kuelekea mahali pengine, na kuamua kwenda kuwakabiliana na Waviking mwenyewe.

Akiwa safarini kuelekea kwa Waviking, akashtukia kama anafuatwa kimya-kimya na bubu anayempenda Ghost. Kule katika kile kijiji kilichoachwa, wameweka mitego kwa mfululizo. Starfire, muda huohuo, ameamua kuondoka kule kabirani na kwenda kumtafuta Ghost na rafiki yake wa karibu. Wakawaua Waviking kwa kuvizia, wakaiba ngao na silaha zao. Pathfinder, naye kama binti yake, pia kaenda kumtafuta Ghost na kujiunga katika mapigano. Ikatokea, yule bubu na Pathfinder kuawa, na Ghost na Starfire waka-kamatwa. Ghost anatambulika kama mtoto wa Viking. Waviking wakatishia kumtesa Starfire iwapo Ghost hatosaliti mahali pengine pa vijiji, hivyo Ghost akaamua kuwasaidia Waviking.

Akapata amana ya Waciking, Ghost akawongoza kwenye njia hatari ya mlima. Gunnar akaamuru kila mmoja wajifunge pamoja ili kupunguza hatari za kila mtu kuanguka kutoka katika mlima mrefu, na Waviking wakafanya kama anavyosema. Wakitumia kwa kuning'inia, halafu Ghost akazua balaa na kupelekea mstari mzima wa Waviking kuanguka chini ya mlima, wale wote waliojifunga pamoja: Gunnar peke yake aliyefaula kukata kamba kwa wakati uliotakiwa.

Baada ya mapigano makali baina ya Ghost na Gunnar kule juu ya mlima, Ghost akamshughulikia kwa kupiga makelele ili mabarafu yaanguke, na kumwacha Gunnar akiwa ananing'inia katika nchi ya kilima, akishikiria na kidani peke yake. Gunnar akaomba umauti kwa kuawa na panga, na kusema kwamba yeye ndiye Ghost pekee aliyebakia katika nchi ile: Ghost akamjibu kwa kutetema kwa baridi "Wewe siyo wa aina yangu" na kukata kile kidani kilichokuwa kikimshikiria Gunnar na kumwacha akianguka katika makolongo, na Mviking huyo kupoteza maisha.

Ghost akarejea kwa Starfire na kidani cha Pathfinder, hivyo na kumfanya Starfire kuwa Pathfinder mpya baada ya baba yake. Ghost akafikiria kwamba ana nafasi ya kuwa kama Mlinzi wa Pwani, shupavu wa kabira lao, kawekwa kuhakikisha kwamba Waviking hawarudi tena.

Marejeo

hariri
  1. "Pathfinder (2006 Film)". The Movie Insider. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-06. Iliwekwa mnamo 2006-12-21.

Viungo vya Nje

hariri