Paul Siniga
Paul Siniga ni mjasiriamali, mwanadiplomasia, na mbobezi wa masuala ya kisera. Amekuwa mwanaharakati wa masuala ya uwezeshaji kwa vijana (youth empowerment) kwa muda sasa. Paul ni mshindi wa malengo ya maendeleo endelevu nchini Tanzania, Balozi wa Udhamini wa kimasomo bara la Uropa, Mwana mabadiliko ya watoto wa Unicef Tanzania, kiongozi aliyepita wa YUNA -Youth of United Nations Association of Tanzania[1].
Paul amefanikiwa kufungua kampuni yake ya masuala ya mitindo na usimamizi wa matukio. kupitia shughuli zake mbalimbali katika jamii, Paul amechaguliwa kuwa katika bodi ya washauri ya mashirika yasiyo ya faida kama vile Global Diplomats Morocco na Africa Youth Transformation Tanzania. Paul ameendelea kushiriki katika masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya jamii na kushiriki katika miradi ya kijamii ambayo imemfanya aendelee kuwa kijana wa kuigwa serikalini, sekta binafsi, balozi mbalimbali na wadau wa masuala ya vijana[2].
Marejeo
hariri- ↑ "The Team - African Reflections Foundation" (kwa American English). 2021-02-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-28. Iliwekwa mnamo 2022-02-28.
- ↑ "The Team - African Reflections Foundation" (kwa American English). 2021-02-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-28. Iliwekwa mnamo 2022-02-28.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paul Siniga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |