Petali
Petali ni majani ya pekee katika ua ambayo huzunguka sehemu za uzazi za ua. Majani hayo pia katika aina kadha za maua huwa na rangi pamoja na harufu nzuri yenye kuvutia wadudu na binadamu. Uwezo wa majani haya kuvutia wadudu huchangia utungishaji yaani umuhimu katika uzazi wa mimea. Petali zote katika ua huitwa corolla.
Kwa kawaida petali hukaa pamoja na seti nyingine ya majani ya pekee ambayo huitwa sepali, ambayo hukaa chini ya muunganiko wa petali. Ingawa petali kwa kawaida huwa ndiyo maeneo dhahiri katika maua yatungishwayo na wanyama, hasa wadudu, spishi za mimea itungishwayo kwa njia ya upepo, hasa majani huwa na petali ndogo mno au hukosa petali kabisa.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Petali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |