Peter Burton (4 Aprili 1921 - 21 Novemba 1989) alikuwa mwigizaji wa filamu na televisheni kutoka mjini Bromley, Uingereza. Madai yake makubwa ya kuwa maarufu ni kwamba yeye ndiye mwigizaji wa kwanza kucheza uhusika wa Major Boothroyd, almaarufu kama Q, katika filamu ya kwanza ya James Bond, Dr. No (1962). Kwa kufuatia mgogoro wa kiratiba, Burton hakupatikana tena katika kuendeleza uhusika huo kwa ajili ya filamu ya From Russia with Love (1963) na kwa maana hiyo nafasi yake ikachukuliwa na mwigizaji wa Q wa muda mrefu, Desmond Llewelyn.

Peter Burton

Burton as Major Boothroyd in Dr. No.
Amezaliwa (1921-04-04)4 Aprili 1921
Bromley, London, England
Amekufa 21 Novemba 1989 (umri 68)
London, England

Burton amepata kuonekana katika vipindi kadhaa vya televisheni ikiwa ni pamoja na The Avengers, The Saint, Return of the Saint, na UFO .

Filmografia zilizochaguliwa

hariri
  • The Bitch (1979)
  • Carry On at Your Convenience (1971)
  • A Clockwork Orange (1971)
  • Lawrence of Arabia (1962)
  • Dr. No (1962)
  • The Iron Maiden (1962)
  • Lugarno (1961)
  • Sink the Bismarck! (1960)
  • They Who Dare (1954)
  • The Heart of the Matter (1953)
  • The Wooden Horse (1950)
  • What the Butler Saw (1950)

Viungo vya Nje

hariri