Peter Petrelli
Peter Petrelli, imechezwa na Milo Ventimiglia, ni jina la kutaja uhusika katika mfululizo wa ubunifu wa kisayansi kupitia televisheni ya NBC - maarufu Heroes. Ni mwuguzi wa jumba la watu mahututi ambaye amegeukia udaktari usaidizi akiwa katikati mwa miaka 20 akiwa na nguvu za kufyonza na kugezea nguvu za watu wengine wenye vipawa.
Peter Petrelli | |
---|---|
muhusika wa Heroes | |
Mwonekano wa kwanza | "Genesis" |
Mwonekano wa mwisho | "Brave New World" |
Imechezwa na | Milo Ventimiglia |
Maelezo | |
Kazi yake | Mwuguzi katika jumba la kupumzikia watu mahututi Mganga-msaidizi (bila taaluma) |
Kipawa | Uwezo wa kunakili au kukopa kipawa cha mtu mwingine kama yupo karibu nae Kipawa cha kuhisi au kusikia maumivu ya mwingine, yaani, kujua unafikiria kitu gani |
Mwepesi kuona jambo na vilevile ana huruma mno, awali uhusika ulionekana kuwa na uhusiano mgumu sana na ndugu yake ambaye ni Nathan. Tangu hapo, Peter Petrelli amekuwa akikabiliana na matokeo dhidi ya maamuuzi yanayotokana na vipawa vyake vinamtaka afanye. Mwanzoni mwa mfululizo wa "Heroes" Peter alifyonza kipawa cha mtu mwenye uwezo wa kuwa bomu linasubiri kulipuka.
Katika hekaheka za wahusika wote wa mfululizo walikuwa katika mbio za kuukoa mji New York City kwa hofu ya Peter atalipuka kama bomu la nyuklia. Dakika kadhaa kabla ya tukio ghafula anatokea ndugu yake Peter ambaye ni Nathan na kupaa nae angani na kuokoa watu wa jiji la New York City.
Viungo vya Nje
hariri- Primatech Paper tracker site Ilihifadhiwa 19 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine.
- Peter Petrelli Ilihifadhiwa 31 Machi 2014 kwenye Wayback Machine. on the Heroes wiki