Genesis (Heroes)
"Genesis" ni sehemu kuu ya kwanza ya mfululizo wa ubunifu wa kisayansi unaorushwa na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes. Sehemu hii imeongozwa na David Semel na kutungwa na Tim Kring. Sehemu hii inaonesha wahusika kadhaa wakuu wanagundua hali za kuwa na vipawa vya ajabu kwa mara ya kwanza, na kujaribu kujua zaidi kuhusu vipawa hivyo. Baadhi ya washiriki, ikiwa ni pamoja na Greg Grunberg na Leonard Roberts, hawajaonekana kwenye kipingele hiki, na kutambulishwa baadaye ndani ya msimu (baadhi ya sehemu ambazo Grunberg awali alishiriki lakini ziliondolewa kabla ya kuanza kurushwa hewani).
"Genesis" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Claire Bennet kwenye treni lilinaloungua. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 1 Sehemu 1 | ||||||
Imetungwa na | Tim Kring | ||||||
Imeongozwa na | David Semel | ||||||
Tayarisho la | 101 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 25 Septemba 2006 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
Muhtasari
haririWatu kadhaa duniani waligundua kama wana nguvu za ajabu kweli. Claire Bennet anaweza kujiponesha majelaha ya mwili wake haraka mno. Isaac Mendez anaweza kuchora picha za matukio ya baadaye. Hiro Nakamura ana uwezo wa kuchezea wakati, kusafiri kupitia wakati, na hata kujihamisha kutoka mahali pa moja kwenda kwingine. Mohinder Suresh anajaribu kuendeleza kazi ya marehemu baba'ke aliyekufa hivi karibuni - kazi ya kutafuta watu wenye vipaji vya ajabu.
Hadithi
haririIkiwa kama sehemu kuu ya mfululizo, "Genesis" inaanzisha hadithi zaidi za wahusika wakuu, ikiwa na msingi kamili wa mfululizo. Robert Canning wa ign.com anaelezea kwamba sehemu hii kama "mapigano machache", lakini kuna "mengi ya kutamanisha kuendelea kutazama."
Kipengele cha kati cha mageuko ya mwanadamu, na uwezekano wa mabadiliko ya wanadamu wenye maajabu, inaanzishwa na muhusika Mohinder Suresh, profesa wa vinasaba mjini Madras, India. Baada ya kupata habari ya kifo cha baba'ke, Chandra Suresh, Mohinder anaenda mjini New York kumaliza kazi utafiti ya Chandra, akiamini ilikuwa sababu iliyopelekea kuawa kwake. Hadithi ya Mohinder pia inaanzisha wazo lililolala la njama zinazohusiana na mauaji ya ma-"heroes". Nyumba kwa baba'ke huko mjini Brooklyn, anasikia sauti (lakini hawezi kuona) ya mtu asiyejulikana anasakasaka kwenye makazi ya baba'ke. Mtu yuleyule baadaye kaenda kwenda taxi ya Mohinder, akimwuliza maswali kadha wa kadha ya mashaka kabla Mohinder hajatoroka.
Isaac Mendez ni msanii na mtawaliwa wa heroin aishiye mjini New York City. Anadai ya kwamba anaweza kuchora picha zenye kuonesha matukio ya baadaye, lakini mwanamke wake, Simone Deveaux, lakini mama anaamini ni athari za dawa za kulevya tu zinamfanya awe vile. Baadaye, kufuatia kujikita dawa kadhaa za kulevya, kachora mfano wa mlupuko wa bomu nyuklia linaangamiza mji wa Manhattan. Niki Sanders, kahaba wa mtandaoni huko mjini Las Vegas, Nevada, anagundua nguvu zake wakati yeye na mtoto wake Micah wanalazimika kutoroka dhidi ya majambazi wanaonyemelea nyumba yao. Wakati wa kutoroka, Niki anaamini kwamba anaone akisi ambayo si yeye. Amemwacha Micah kwa rafiki yake na kurudi nyumbani, ambapo wale majambazi wakamdaka na kumlazimisha amwagie vimbwanga vya ukahaba wakati wao wanamtazama. Kipengele hiki anaonekana kuzilai wakatia anacheza, kuamka baadaye kakuta wale watu wameauwa kikatili na mtu asiyejulikana. Akisi yake ya ajabu inamwonesha anyamaze kimya. Wote wawili Isaac na Niki wanagundua nguvu zao kuwa "si za kuzikaribisha hivyo basi lazima wanashughulikie na waondokane nazo."
Marejeo
haririViungo vya Nje
hariri- Watch "Genesis" at NBC.com
- Genesis at the Internet Movie Database
- Beaming Beeman: Episode 1: Genesis Director's blog on the filming of this episode.