Phaswane Mpe

Mwandishi wa Afrika Kusini (1970-2004)

Phaswane Mpe (10 Septemba 1970 - 12 Desemba 2004) alikuwa raia wa Afrika Kusini mshairi na mwandishi wa riwaya.

Alisoma katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, ambapo alikuwa mhadhiri wa fasihi ya Kiafrika. Alisoma digrii ya uzamili katika maswala ya kuchapisha katika Chuo Kikuu cha Oxford Brookes. Mnamo mwaka 1998 riwaya yake ya ya kwanza ijulikanayo kama, Welcome to Our Hillbrow, ilichapishwa katika 2001 . Mikusanyiko ya hadithi fupi na mashairi yake , Clouds Brooding, yalichapishwa baada ya yeye kufa mnamo mwaka 2008.

Mpe alizaliwa katika mji wa kaskazini wa Polokwane huko Tiragalong,[1]na kuhamia Johannesburg akiwa na umri wa miaka 19 alifanikiwa kujiunga na chuo kikuu. Kwa sababu ya ukosefu wake wa pesa aliishia kuishi katika eneo la ndani la jiji la Hillbrow, mahali ambapo baadaye aliandaa riwaya yake ya kwanza ijulikanayo kama Welcome to Our Hillbrow ilikuwa kazi muhimu kwake kwani ilikuwa riwaya ya kwanza kushughulikia mabadiliko ya maisha ya ndani huko nchini Afrika Kusini ndani ya miaka kumi tangu Nelson Mandela na F. W. de Klerk kuangamiza ubaguzi wa rangi. Kitabu hiki kinawaonyesha Waafrika Kusini weusi wakikabiliwa na changamoto za umaskini, ukosefu wa ajira, na VVU / UKIMWI. Riwaya hiyo inashangaza kwa kuwa shida zilizoundwa na ubaguzi wa rangi hazikuwa zinajulikana ; shida kuu za Waafrika Kusini weusi ni zile za kujitengenezea wao: chuki dhidi ya wageni, uvumi wa roho mbaya, uchawi, na kutoweza kupendana kabisa au kujipenda wenyewe.

Labda ilikua haishangazi, kwa kuzingatia kuenea kwa ugonjwa huo nchini Afrika Kusini, VVU na UKIMWI zilikuwa mada za kawaida katika kazi ya Mpe. Kabla ya kifo chake alianza masomo ya udaktari kuhusu jinsia katika fasihi ya Afrika Kusini, baada ya ubaguzi wa rangi na alikua akizingatia sana masuala haya mawili.

Mpe alikufa ghafla akiwa na umri wa miaka 34, wakati huo alikuwa anajiandaa kuanza mafunzo kama mganga wa kienyeji.

Wakati mauti ikimkuta, Mpe alikuwa akifundisha fasihi ya Kiafrika na masomo ya uchapishaji katika fasihi na masomo ya lugha katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Mashairi yake na hadithi fupi zimechapishwa katika Imprint (1995), Staff Rider (1980). Alichangia pia hadithi fupi katika Jarida la Drum.

Kitabu chake cha Welcome to Our Hillbrow, na hadithi fupi katika Clouds Clouds zina habari kubwa za kihistoria.[2]

Marejeo hariri

  1. Mpe Phaswane. 2001.Welcome To Our Hillbrow.
  2. Mpe, P. 2001. Welcome To Our Hillbrow
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Phaswane Mpe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.