Piflufolastati F-18
Piflufolastati F-18 (Piflufolastat F-18), inauzwa kwa jina la chapa Pylarify, ni ajenti ya utambuzi inayozalisha nishati kutokana na kuoza kwa viini vya aina fulani za atomi na isotopu inayotumika katika upigaji picha wa tomografia ya positron emission (PET).[1] Hasa inatumika kupiga picha ya saratani ya tezi dume ambayo ni antijeni maalumu ya utando wa tezi dume (PSMA) ili kuangalia kuenea au kujirudia kwake.[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudungwa sindano kwenye mshipa.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, mabadiliko ya ladha, na uchovu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio na kuathirika ka mnururisho.[1]
Piflufolastati F-18 iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2021.[1] Haikuidhinishwa kwa ajili ya matumizi Ulaya wala Uingereza kufikia mwaka wa 2022.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Pylarify- piflufolastat f-18 injection". DailyMed. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 12 Septemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Piflufolastati F-18 kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |