Plekanatidi
Plekanatidi (kwa Kiingereza: Plecanatide), inayouzwa kwa jina la chapa Trulance, ni dawa inayotumika kutibu kuvimbiwa choo kwa muda mrefu na kuvimbiwa choo kwa kawaida kwa sababu ya ugonjwa wa matumbo ya kuwasha.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara.[1] Haipendekezwi kuitumia kwa watoto.[2] Usalama wake katika ujauzito hauko wazi.[3] Dawa hii hufanya kazi kwa kuwezesha kimeng'enya cha guanylate cyclase-C ambacho huongeza kutolewa kwa kloridi na baikaboneti (bicarbonate) ndani ya utumbo.[2]
Plekanatidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017.[1] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 470 kwa mwezi.[4]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "DailyMed - TRULANCE IMMEDIATE RELEASE- plecanatide tablet". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "Plecanatide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Plecanatide (Trulance) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Plecanatide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)