Povu (ing. foam) ni viputo au matone ya hewa au gesi yoyote vilivyofunga katika kiowevu au dutu manga.

Povu ya zabuni

Mifano yake ni povu ya sabuni, sifongo, povu ya plastiki inayotumiwa kama godoro, au fuwawe ambayo ni povu ya mwamba.

Kuta nyembamba za kiowevu au dutu manga zinatenganisha nafasi zinazojaa gesi.