Fuwawe
Fuwawe (pia: fuwe; ing. pumice) ni aina ya mwamba mwepesi inayoundwa na povu ya zaha (lava).
Maana yake zaha ambayo ni mwamba joto sana katika hali ya kiowevu inarushwa kutoka volkeno kwa shinikizo kubwa inakuwa kama povu kwa sababu shinikizo inapungua haraka sana. Ikipoa haraka umbo hili linaganda kuwa thabiti na kubaki vile.
Kwa hiyo asili ya fuwawe ni daima mlipuko wa volkeno.
Fuwawe inatokea kama mkusanyiko wa vipande-vipande au pia kama maganda manene.
Mara nyingi ni nyepesi kiasi inaelea juu ya maji, angalau kwa muda hadi maji yanaingia na kujaza polepole nafasi ndani yake.
Kiasili inatumiwa kwa kusugua na kusafisha ngozi. Fuwawe iliyosagwa inatumiwa pia kwa kusafisha meno kwa msaada wa mswaki.
Kuna pia matumizi ya fuwawe kwa ujenzi maanake ni kifaa chepesi chenye tabia nzuri za kuhami dhidi ya baridi na joto. Kwa kawaida inapondwa, kuchanganywa na kiasi kidogo cha saruji[1] lakini kuna pia majaribio ya kuitumia vile.[2]
Marejeo
hariri- ↑ When technology fails - Pumice Crete, uk. 161, via google books, ilitazamiwa Juni 2016
- ↑ Building with pumice
Viungo vya Nje
hariri- University of Oxford image of pumice. Ilihifadhiwa 26 Julai 2020 kwenye Wayback Machine. Retrieved 2010-09-27.
- Analytical identification of a single source pumice from Greek shores and ancient sites in the Levant
- On the occurrence of a pumice-rich layer in Holocene deposits of western Peloponnesus, Ionian Sea, Greece. A geomorphological and geochemical approach.