Radha Poonoosamy (18 Septemba 1924Januari 2008) alikuwa mwanasiasa wa Mauritius, waziri wa kwanza mwanamke kwenye baraza la mawaziri nchini humo na mwanaharakati wa masuala ya wanawake.

Alizaliwa Radha Padayachee tarehe 18 Septemba 1924 huko Durban Afrika Kusini. Alizaliwa katika familia ya asili ya Kihindi.

Alisoma katika Chuo Kikuu cha Natal, ambapo alikuwa "mpinzani mkubwa wa ubaguzi wa rangi" na akawa mwanachama wa Baraza la Wanafunzi la "Indian National Congress" ambalo lilipigana dhidi ya ubaguzi wa wahindi nchini Afrika Kusini.Aliendelea kuwa mkuu wa sehemu ya wanawake na pia mjumbe wa kamati kuu ya African National Congress (ANC).

Aliolewa na daktari Dkt. Valaydon Poonoosamy wakaishi Mauritius mwaka 1952. Akawa raia nchini humo na kuendeleza harakati zake huko ndani ya Chama cha Labour cha Mauritius.

Mnamo mwaka wa 1975, Poonoosamy alichaguliwa kuwa Mbunge, na kuwa waziri wa kwanza mwanamke nchini humo. Waziri mkuu aliyesimamia Wizara ya Masuala ya Wanawake na kusaidia kupitisha sheria dhidi ya ubaguzi wa kijinsia.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Radha Poonoosamy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.