Rafiki (Filamu 2018)

Rafiki[1] ni filamu kutoka nchi ya Kenya iliyotengenezwa katika mwaka 2018. Filamu imeongozwa na Wanuri Kahiu ambaye ni Mkenya. Yeye aliandika “Rafiki” na Jenna Bass, meneja wa cinema kutoka Afrika ya Kusini.

Rafiki
Imeongozwa na
Wanuri Kahiu[2]
Imetayarishwa na Steven Markovitz
Wasanii Wanuri Kahiu

Jena Cato Bass

Nyota Samantha Mugatsia

Sheila Munyiva

Sinematografi Christopher Wessels
Imehaririwa na Isabelle Dedieu
Imetolewa tar. 9 May 2018 (Cannes)

23 September 2018 (Kenya)

Ina muda wa dakika 82
Nchi Kenya
Lugha Kiingereza

Kiswahili

Mauzo ya Ofisi $176,513[3]


Hadithi hariri

“Rafiki” inahusu wanawake wawili, Kena na Ziki, ambao walianza kupendana. Kena alitoka jiji la Nairobi na alikaa katika nyumba ya mama yake, lakini husaidia katika duka la baba yake. Baba ya Kena alifanya kampeni katika uchaguzi wa serekali ya mtaa. Wakati wa kufanya kazi, Kena alianza kuonyesha mapenzi na Ziki, mwanamke wa mtaa. Lakini, Ziki ni binti la Peter Okemi, mshindani wa baba ya Kena katika uchaguzi wa serekali ya mtaa.  Hata hevyo, Ziki na Kena waliendelea mchezo wa datsi nyingi na walikuwa karibukaribu sana. Lakini hawaweza kuonyesha uhusiano wao kwa sababu usenge ni haramu katika nchi ya Kenya.

Marafiki wa Ziki walikasirika kwa sababu yeye hutumia wakati mwingi na Kena kwa hivyo walimpiga Kena. Kisha, Ziki alisaidia kupona Kena katika nyumba ya Ziki lakini mama ya Ziki aliona, wakati alienda chumbani, wakibusu. Walijaribu kukimbia lakini kundi la watu wenye waliwapata. Wamekamatwa, kisha wazazi wao walikuja kuwachukua. Baddaye, wazazi wa Ziki wanampeleka jiji la London na wazazi wa Kena walificha hali hiyo yote. Mwisho wa filamu, miaka kadhaa baadaye, Ziki alirudi mtaa na alikutana na Kena tena. Kena alimaliza shule wakaanza tena uhusiano wao.

Washiriki hariri

• Samantha Mugatsia ni Kena[4]

• Sheila Munyiva ni Ziki

• Neville Misati ni Blacksta

• Nini Wacera ni Mercy

• Jimmy Gathu ni John Mwaura

• Charlie Karumi ni Waireri

• Muthoni Gathecha ni Mama Atim

• Dennis Musyoka ni Peter Okemi

• Patricia Amira ni Rose Okemi

• Nice Githinji ni Nduta

• Patricia Kihoro ni Josephine

• Mellen Aura ni Elizabeth

Mapokezi hariri

Wakati filamu "Rafiki" ilitolewa watu hawakuruhusiwa kuitazama katika nchi ya Kenya kwa sababu Bodi ya Uainishaji Filamu Nchini Kenya (KFCB) walipiga marufuku filamu[5]. KFCB walisema ni marufuku kwa sababu ya mada yake ya ushoga na dhamira ya wazi ya kukuza usagaji nchini Kenya kinyume na sheria. Bodi waliomba Wanuri Kahiu abadilishe mwisho wa filamu usiwe tumaini lakini Kahiu alisema hapana. Kwa hiyo, KFCB walionya watu kwamba wakinunua filamu wanaweza kuenda jela. Wapigania haki za ushoga wa kimataifa walikasirika.[6] Kisha, Wanuri Kahiu alidai serikali ya Kenya kwa sababu alitaka kuingia Tuzo la Chuo (Academy Award) cha Filamu Bora ya Lugha ya Kigeni kwa mwaka tisini na moja za maadhimisho[7].

Mnamo 21 Septemba 2018, Mahakama Kuu ya Wakenya iliondoa marufuku ya filamu kwa siku saba[8].[9] Baada ya marufuku kutolewa, “Rafiki” iliuzwa kabisa kutoka sinema katika jiji la Nairobi[10]. Lakini, hata hivyo, “Rafiki” haikuenda Tuzo la Chuo.

Marejeo hariri

  1. "RAFIKI". Festival de Cannes 2019 (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  2. "Kenyan Director Wanuri Kahiu Is Fun, Fierce, Frivolous and Timely". The Hollywood Reporter (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  3. "Rafiki (2018) - Financial Information". The Numbers. Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  4. "What I Learnt from My Lesbian Role in "Rafiki"- Samantha Mugatsia". Eelive (kwa en-US). 2019-03-13. Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  5. "Lesbian film banned ahead of Cannes debut", BBC News (kwa en-GB), 2018-04-27, iliwekwa mnamo 2020-03-05 
  6. "Ban of Kenyan film over lesbianism criticised". Daily Nation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  7. Mumbi Mutuko on 11 September 2018-6:45 pm. "Govt Sued for Preventing Kenyan Movie From Winning Oscars". Kenyans.co.ke (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  8. Tuko.co.ke (2018-09-21). "High Court lifts ban on lesbian movie, dismisses moral police Ezekiel Mutua". Tuko.co.ke - Kenya news. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  9. "High court lifts ban on lesbian themed movie 'Rafiki'". The Star (kwa en-KE). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 
  10. Cecilie Kallestrup (2018-09-23). "Lesbian film Rafiki sells out after Kenyan court lifts ban". The Sydney Morning Herald (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-05. 

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rafiki (Filamu 2018) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.