Raisin Bran
Raisin Bran (au Sultana Bran katika baadhi ya nchi) ni chakula cha aina ya nafaka kinacholiwa kama kiamshakinywa. Kimepikwa hasa kwa kutumia nafaka,bran na zabibu zilizokaushwa(raisin). kinachotayarishwa na kampuni kadhaa chini ya majina mbalimbali kama :Kellogg's Raisin Bran, General Mills' Total Raisin Bran,toleo la General Mills linaloitwa Raisin Nut Bran na Kraft Foods' Post Raisin Bran.
Skinner's Raisin Bran ni aina ya kwanza ya bidhaa hii iliyofika kwenye soko, ilianza kuuzwa katika soko la Marekani katika mwaka wa 1926 na kampuni ya US Mills,inayojulikana zaidi kama nafaka ya Uncle Sam. Jina hilo la "Raisin Bran" lilikuwa ,wakati mmoja,lilikuwa karibu kushikiliwa kisheria na kampuni moja lakini kesi hii ilizua mgogoro kuhusu bidhaa za aina zozote zilizotayarishwa kwa kutumia nafaka,bran na zabibu zilizokaushwa zilizotaka kutumia jina hilo. Hatimaye, ilionekana kuwa bran na zabibu zilizokaushwa hutumika sana katika utayarishaji wa nafaka na jina hilo lilitumika sana.Hivyo basi likawa huru kutoka sheria zozote za kullifunga kwa kampuni yoyote.
Historia
haririHivi leo, bidhaa ya aina hii inayojulikana sana ni Kellog's Raisin Bran, ilianzishwa katika mwaka wa 1942. Bidhaa hii ya Kellog's inajulikana sana kwa kaulimbiu yake ya matangazo: "Vijiko viwili vya zabibu zilizokaushwa za Kellogg's Raisin Bran ni vizuri" na pia kwa katuni iliyowakilisha bidhaa hiyo.Katuni hii ilikuwa juu iliyowaka na iliitwa "Sunny" iliyoanzishwa 1966. Kellogg's sasa ina bidhaa mbalimbali za aina iliyoitwa Raisin Bran Crunch , iliyohusisha nafaka na asali. Bidhaa hii inajulikana kwa kuwa na vinyuzinyuzi vingi na hushutumiwa kwa kuwa na sukari nyingi sana. Zabibu zilizokaushwa zina asili ya kuwa na sukari nyingi. Aidha, kuzuia kushikana katika upishi,watayarishaji huongeza sukari kwa zabibu hizo: tangu 7 Januari 2010 ,Kellog's huongeza mchuzi wa mahindi wenye sukari nyingi kwa nafaka yake ya Raisin Bran. Zabibu hizi,ambazo huwa takriban elfu katika kila pakiti, huwa 60% ya uzito wa nafaka hii.
Nyimbo zilizotumika
hariri- Wimbo wa "The sunniest brand under the sun" (ulitumika kuanzia mwaka wa 1965 hadi wa 1970)
- Wimbo wa "Two scoops of raisins in a box of Kellogg's Raisin Bran." (Marekani, ulitumika kuanzia miaka ya 1970 hadi 1990)
- Wimbo wa "Two scoops of raisins in a package of Kellogg's Raisin Bran" (Kanada,ulitumika hadi 1993, ulianza kutmika tena katika mwezi wa Oktoba 2006)
- Wimbo wa "Two scoops of raisins, in Kellogg's Raisin Bran" (Kanada, ulitumika katika katikati na mwisho wa miaka ya 1990)
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Sultana Bran Ilihifadhiwa 17 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
- All-Bran Sultana Bran Ilihifadhiwa 24 Septemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- A quantitative analysis of Kellogg's Raisin Bran (Science Creative Quarterly)