Rajery jina lake kamili ni Germain Randrianrisoa, ni mchezaji wa valiha kutoka Madagaska ambaye alianzisha orchestra ya kisasa ya valiha.[1] [2]Akiwa mtoto mdogo (miezi 11 ), alipoteza vidole vyote kwenye mkono wake mmoja, akiwa kwenye harusi aliyokwenda akiwa na wazazi wake[3] baadaye, akawa mchezaji wa valiha aliyejifundisha mwenyewe.[4]

Wasifu

hariri

Rajery alizaliwa mwaka wa 1965 huko Madagaska kaskazini.[5] Akiwa kijana, alitaniwa na rika lake kwa kutaka kucheza valiha, chombo ambacho kwa kawaida huhitaji matumizi mengi ya mikono yote miwili. Hata hivyo, kutokana na ulemavu wake, alibuni mbinu na mtindo wa kipekee wa muziki[5]. Kwa wakati huu, hapakuwa na njia ya kupata maelekezo rasmi ya kucheza valiha. Rajery alifanya kazi ya kutatua tatizo hili kupitia uandishi wake wa kitabu Siri ya Valiha, ambacho kilijumuisha pia mfumo wa nukuu za muziki. Tangu 2006, Rajery amekuwa mwanachama wa kundi la watatu la muziki ya 3MA, ambayo yeye hutembelea na kurekodi.[5]

Diskografia

hariri
  • Dorotanety (Indigo, Label Bleu, 1999)[6]
  • Fanamby (Indigo, Label Bleu, 2001)[6]
  • Anarouz (Six Degrees Records, 2017, as a member of 3MA)[5]

Marejeo

hariri
  1. https://www.allmusic.com/artist/rajery-mn0000394261/biography
  2. https://www.smallislandbigsong.com/rajery
  3. https://www.allmusic.com/artist/rajery-mn0000394261/biography?1651401983900
  4. https://worldmusiccentral.org/tag/rajery/
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 https://www.theadvocate.com/gambit/new_orleans/events/stage_previews_reviews/article_a633559c-96bd-5262-9f02-27b8d5c011d3.html
  6. 6.0 6.1 https://mg.co.za/article/2003-06-10-malagasy-musician-revives-tradition/