Ramia ni kifaa kinachounganisha risasi na baruti kwa matumizi katika silaha ya moto.

Ramia
Ramia ya kisasa huwa na:
1) risasi yenyewe
2) ganda la ramia; mara nyingi ni ya metali
3) baruti au kemikali yenye uwezo wa kuwaka haraka mara moja ikitoa gesi
4) mguu wa ganda ni pana kwa kushikilia ramia kwenye chemba ya silaha
5) kiwashio ni kemikali linalowaka ikipigwa na moto yake inawasha baruti


Zamani silaha za moto zilijazwa kupitia mdomo wa silaha kwa kuingiza baruti na risasi pekee.

Ramia inaunganisha yote pamoja.

Sehemu za ramia

hariri

Risasi

hariri

Kwa habari za undani zaidi tazama makala ya risasi

Risasi yenyewe hubanwa mbele katika ganda.

 
Sehemu za ramia: Risasi, baruti, ganda na kiwashio

Ganda la ramia

hariri

Ganda hili mara nyingi ni ya metali ama shaba nyeupe au feleji. Kwa mazoezi kuna pia maganda ya plastiki. Ramia ya bunduki ya marisau huwa pia na ramia ya karatasi ngumu kwa sababu hapa risasi ni ya vipande vingi kidogo isiyobanwa na ganda bali viko ndani ya ramia.

Baruti

hariri

Baruti ni kiasi kinachohitajika kwa kurusha risasi kulingana na uwezo wa silaha. Baruti ina uwezo wa kulipuka yaani ya kuchomeka haraka na ghafla iikitoa gesi zinasopanua na kusukuma risasi. Lakini baruti haitakiwi kuwa nyororo mno; ramia sharti ni kuvumulia pigo na mishtuko bila kulipuka. Aina kali sana za baruti zinafaa kwa mlipuko katika uwindo wa mawe bali si kwa ramia.

Kiwashio cha ramia

hariri

Kazi ya kuwasha baruti hutekelezwa na kiwashio ambacho ni kiasi kidogo cha kemikali kinachowaka moto ikipigwa vikali. Hufungwa katika silinda ndogo ndani ya mguu wa ramia. Mguu huu unapigwa na msumali wa bunduki na kuwaka moto inayowasha baruti.

Mengineyo

hariri

Ramia kwa ajili ya mazoezi kwa mfano kuzoea makelele au kwa matumizi katika filamu hukosa risasi lakini zinatoa kelele na moto kama ramia ya kawaida.

Ramia kubwa za mzinga mara nyingi huitwa "kombora" lakini neno hili latumiwa pia kwa "roketi".

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: