Baruti ni kilipukaji ambacho ni mchangayiko wa dutu za kikemia unaotumiwa kurusha risasi kutoka bunduki. Ina mmenyuko wa haraka kati ya kemikali zake ikipashwa moto inatoa gesi nyingi. Kama mmenyuko huo unatokea penye nafasi kubwa inachoma haraka na ghafla lakini kama unatokea mahali unapobanwa kuna mlipuko. Kwa hiyo baruti ni kilipukaji.

Baruti nyeusi

Tabia hii inatumiwa kurusha risasi kutoka silaha za moto. Gesi ya mlipuko zinapanua zikifuata nafasi ya pekee inayopatikana kwenye kasiba ya bunduki kueleka mdomo wake. Risasi iliyopo mbele inasukumwa na kupata mbio.

Baruti iligunduliwa na Wachina mnamo mwaka 1200. Kuna taarifa kutoka karne ya 13 kuhusu matumizi ya baruti kwa mabomu vitani. Kutoka China teknolojia ya baruti ilienea magharibi kupitia Waarabu na kufika Ulaya katika karne ya 13.

Aina asilia ya baruti ilikuwa baruti nyeusi inayotengenezwa kwa kuchanganya nitriti ya potasiamu, makaa na sulfuri. Inachoma kwa moshi mwingi na nguvu yake ni hafifu kulingana na baruti za kisasa. Siku hizi hutumiwa tu katika fataki za burudani.

Baruti za kisasa ziligunduliwa Ulaya wakati wa karne ya 19. Wanajeshi walizipendelea kwa sababu zililipuka bila moshi. Nguvu ya mlipuko iliongezeka iliyomaanisha ya kwamba kiasi kidogo cha baruti kilitosha; risasi zilifika mbali zaidi na wanajeshi waliweza kubeba ramia nyingi kuliko awali.


Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baruti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.