Ranga Chivaviro
Ranga Chivaviro (amezaliwa 21 Novemba 1992) ni mchezaji wa soka wa Afrika Kusini anayesakata mpira wa miguu katika klabu ya Marumo Gallants ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, akiwa kama mshambuliaji. Alizaliwa Limpopo, na mama wa Afrika Kusini na baba wa Zimbabwe.
Historia ya Klabu
haririChivaviro alicheza kwa klabu za Witbank Spurs, Cape Town All Stars, na Ubuntu Cape Town kabla ya kusaini na klabu ya Baroka ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu wa kiangazi wa mwaka 2018. Baada ya kusalia kwa mkopo katika klabu ya TS Sporting katika msimu wa 2019-20, alitolewa na Baroka mwishoni mwa msimu.
Mwezi Machi 2021, Chivaviro alisaini na klabu ya KF Trepça '89 ya Kosovo.[6] Aliondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Mwezi Septemba 2021, alirudi Afrika Kusini na kusaini na Venda FA. Aliondoka katika klabu hiyo mwezi Juni 2022.
Mwezi Agosti 2022, Chivaviro alihamia Marumo Gallants[8] na alikuwa sehemu ya kikosi cha Gallants kilichofanikiwa kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF kwa msimu wa 2022-23.
Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali, Gallants walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Pyramids huko Cairo. Chivaviro aliiwezesha Gallants kuongoza kwa bao 1-0 mapema katika kipindi cha pili, lakini Pyramids walifanikiwa kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti katika dakika za mwisho za mchezo. Katika mchezo wa marudiano nchini Afrika Kusini, Gallants walishinda 1-0 na kuhakikisha nafasi yao katika nusu fainali.
Gallants walikutana na Young Africans, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu wa 2021-22, katika nusu fainali yenye mechi mbili. Katika mchezo wa kwanza huko Tanzania tarehe 10 Mei, Young Africans waliongoza kwa 2-0, wakifunga mabao mawili katika kipindi cha pili.
Kabla ya mchezo wa marudiano, Chivaviro na Fiston Kalala Mayele wa Young Africans ni wafungaji bora wa Kombe la Shirikisho la CAF kwa msimu wa 2022-23, kila mmoja akiwa amefunga magoli matano.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ranga Chivaviro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |