Rania Al Abdullah (Kiarabu: الملكة رانيا العبد اللهRānyā al-‘abdu l-Lāh; alizaliwa 31 Agosti 1970) ni mke wa Mfalme Abdullah II wa nchi ya Jordan.

Rania Al Abdullah

Yeye anachukuliwa mojawapo ya wanawake majabari kote duniani[1]. Rania ametumia nguvu zake kuhimiza umuhimu wa elimu.

Nchini Jordan, kazi yake inahusu kutathmini kiwango cha elimu ya wanafunzi, na akiwa nje ya nchi anawahimiza viongozi kuhusu elimu.

Maisha ya kibinafsi

hariri

Rania Al-Yassin alizaliwa nchini Kuwait kutokana na wazazi wa Kipalestina mjini Tulkarm. Alisoma shule ya msingi na ya upili katika New English School, Kuwait, kisha akafuzu kwa shahada ya biashara kutoka chuo kikuu cha American University in Cairo. Alipofuzu, Rania alirudi Jordan na kufanya kazi kwenye benki ya Citibank, na baadaye akafanya kazi kwenye kampuni ya kompyuta iitwayo Apple Computer mjini Amman.[2]

Ndoa na watoto

hariri

Alikutna na Mfalme Abdullah bin Al-Hussein kwenye sherehe mnamo Januari 1993. Baada ya miezi miwili, alikuwa mhumba wake na walioana mnamo 10 Juni 1993. Wana watoto wanne:

  • Hussein bin Al Abdullah (alizaliwa 28 Juni 1994)
  • Iman bint Al Abdullah (alizaliwa 27 Septemba 1996)
  • Salma bint Al Abdullah (alizaliwa 26 Septemba 2000)
  • Hashem bin Al Abdullah (alizaliwa 30 Januari 2005)

Malkia wa Jordan

hariri

Ingawa mumewe alikuwa mfalme tangu 7 Februari 1999, Rania hakuwa malkia papo hapo. Mumewe alimtuza Umalkia mnamo 22 Machi 1999.[3]

 
Michelle Obama na Rania wakiwa kwenye ikulu ya White House mnamo 23 Aprili 2009

Rania alianzisha tume ya Jordan River Foundation mnamo 1995 ambayo inaboresha familia na jamii maskini kwa kuwafundisha jinsi ya kuanzisha biashara.[4]

Mnamo 2009, Rania na mumewe walisherehekea miaka kumi ya ndoa yao kwa kuanzisha mashindano ya jamii (Ahel Al Himmeh) mnamo Machi ili kuwatuza watu ambao wamesaidia jamii yao.[5]

Tovuti

hariri

Rania anadai kuwa yeye ni mwanateknolijia ambaye unaweza kumpata kwenye tovuti kama YouTube, Facebook na Twitter.

YouTube

hariri

Mnamo Machi 2008, Rania alianzisha YouTube channel na kuwaalika watazamaji waulize maswali walionayo kuhusu Uislamu.[6]

Pia, ameweka mahojiano yake ya CNN kwenye YouTube, ambap alizungumzia kuhusu elimu.[7]

Facebook

hariri

Rania ni mshiriki wa Facebook ambapo ameweka picha zake akiwa nyumbani na akiwa hadharani. Hadi 17 Desemba 2009, alikuwa na mashabiki 110,000.

Twitter

hariri

Mnamo Juni 2009, Rania alishiriki kwenye mahojiano ya Twitter, alipojibu maswali matano kutoka kwa umma.[8]

Marejeo

hariri
  1. The 100 Most Powerful Women: #76 Queen Rania, Forbes Magazine, 19 Agosti 2009.
  2. "Profile: Jordan's Queen Rania", BBC 7 Novemba 2001.
  3. "King proclaims Rania Queen". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-05. Iliwekwa mnamo 2010-01-27.
  4. "Jordan River Foundation". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-15. Iliwekwa mnamo 2010-01-27.
  5. "Ahel Al Himmeh". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-16. Iliwekwa mnamo 2010-01-27.
  6. Queen Rania Launched YouTube Channel, USA Today, 31 Machi 2008.
  7. Queen: Education a top priority, YouTube, 25 Aprili 2009.
  8. Twitter interview with Queen Rania Ilihifadhiwa 18 Desemba 2011 kwenye Wayback Machine., World Economic Forum, 12 Mei 2009.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rania Al Abdullah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.