Regia Mtema

wabunge wa Tanzania

Regia Estelatus Mtema (1980-2012) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania. Alikuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira.[1].

Historia

hariri

Mtema alizaliwa tarehe 21 Aprili 1980,[2] . binti wa Estelatus Mtema. [3]

Alisoma katika Shule ya Sekondari ya Forodhani ya jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Machame kwa ajili ya elimu ya sekondari ya juu. Alihitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika uchumi na lishe ya Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).[2]

Alikuwa mwanamke mlemavu, alikuwa hai katika Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania, akiwawakilisha katika warsha ya 2008. Pia alikuwa afisa mkuu katika Kurugenzi ya Masuala ya Vijana ya Chadema. [4].[2]

Mtema alifariki katika ajali ya gari tarehe 14 Januari 2012. [1] Alizikwa Ifakara, Wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.[2] .[5].

marejeo

hariri
  1. https://www.youtube.com/watch?v=WTwldvBKMqM
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Polycarp Machira and Julieth Ngarabali, Chadema MP dies in car crash Ilihifadhiwa 5 Julai 2020 kwenye Wayback Machine., The Citizen, 15 January 2012. Accessed 4 July 2020.
  3. Dora Tesha, Tanzania: Kikwete, Pinda Mourn Chadema MP, Tanzania Daily News, 16 January 2012. Accessed 4 July 2020.
  4. Workshop Report: Research in the stakeholder dialogue on education, gender and inclusion Ilihifadhiwa 17 Oktoba 2022 kwenye Wayback Machine., 20 February 2008. Accessed 4 July 2020.
  5. John Nditi, Tanzania: Kikwete Leads Hundreds At Regia Mtema's Burial in Ifakara, Tanzania Daily News, 19 January 2012. Accessed 4 July 2020.