Rehani
Rehani (toka Kiarabu c رَهْن, rahn) hutumiwa ama na wanunuzi wa mali isiyohamishika ili kupata fedha za kununua mali hiyo; au wamiliki wa mali isiyohamishika ili kuongeza fedha kwa madhumuni yoyote.
Mali ya mkopaji huwekwa rehani ili kulinda maslahi ya mkopeshaji. Hii inamaanisha kuwa kisheria mkopeshaji atakuwa na haki ya kutwaa mali iliyowekwa rehani pale mkopaji atakaposhindwa kulipa.
Waweka rehani wanaweza kuwa ni watu binafsi wanaoweka nyumba zao rehani au kampuni za biashara zinazoweka rehani majengo yao.
Mkopeshaji kawaida huwa ni taasisi ya kifedha, kama vile benki kulingana na nchi husika. Masharti ya mikopo kama ukubwa wa mkopo, ukomavu wa mkopo, kiwango cha riba, njia ya kulipa mkopo, na sifa nyingine huwa zinatofautiana sana.
Haki za wakopeshaji juu ya mali iliyowekwa rehani inachukua kipaumbele zaidi ya wakopaji wengine. Hii ina maana kuwa mkopaji akifilisika, wadai wengine watalipwa tu madeni waliopewa kutokana na uuzaji wa mali iliyowekwa rehani ikiwa mkopeshaji wa mikopo amelipwa kwanza.
Katika nchi nyingi, ni kawaida kwa ununuaji wa nyumbani kufadhiliwa na rehani. Watu wachache wana akiba ya kutosha ili kuwawezesha kununua mali isiyohamishika.
Katika nchi ambapo mahitaji ya umiliki wa nyumba ni ya juu, masoko makubwa ya rehani yameendelezwa.
Rehani zinaweza kufadhiliwa kwa njia ya sekta ya benki (yaani, kwa njia ya amana za muda mfupi), au kwa njia ya masoko ya mitaji.
Viungo vya nje
hariri- Rehani kwenye tovuti ta DMOZ Archived 26 Oktoba 2017 at the Wayback Machine.
- Juu ya rehani Afrika
- Maelezo zaidi juu ya rehani
- Kwanini ni vigumu kumiliki mali isiyohamishika Afrika?
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rehani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |