Mali
Mali (kwa Kifaransa: République du Mali = Jamhuri ya Mali) ni nchi ya Afrika ya Magharibi.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Taifa moja, Lengo moja, Imani moja (Kifaransa: Un peuple, un but, une foi) | |||||
Wimbo wa taifa: Pour l'Afrique et pour toi, Mali (Kwa Afrika na kwako, Mali) | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Bamako | ||||
Mji mkubwa nchini | Bamako | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali | Jamhuri Bah Ndaw Moctar Ouane | ||||
Uhuru Tarehe |
kutoka Ufaransa 22 Septemba 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,240,192 km² (ya 24) 1.4% | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 2009 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 67) 14,517,176 11.7/km² (ya 215) | ||||
Fedha | CFA franc (XOF )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC0) (UTC+1) | ||||
Intaneti TLD | .ml | ||||
Kodi ya simu | +223
- |
Imepakana na Algeria, Mauretania, Niger, Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Senegal. Mali. Haina pwani kwenye bahari yoyote.
Sehemu ya juu ni mlima wa Hombori Tondo (mita 1155 juu ya UB) ulioko katikati ya nchi.
Kaskazini sehemu kubwa ya eneo la Mali ni jangwa la Sahara.
Wakazi walio wengi huishi kusini, karibu na mito Senegal na Niger.
JiografiaEdit
Theluthi mbili za eneo la Niger ni jangwa. Maeneo mengine ni ya Sahel na kanda la Sudan. Sehemu za kusini ni hasa tambarare za bonde la mto Niger.
Hali ya hewa ni tofautitofauti, kulingana na eneo. Kuna kanda tatu:
- Kanda la jangwani kaskazini - usimbishaji chini ya mm 100 kwa mwaka, yabisi na yabisi sana. Hapa wanaishi wafugaji pekee.
- Kanda la Sahel: mbuga nusu yabisi inayobadilika kuwa savana kusini kwenye mvua zaidi. Kuna kilimo kando ya mto Niger.
- Kanda la Sudan lina usimbishaji wa mm 1400 . Lina savana ilhali miti inaongezeka hadi kufika hali ya misitu kabisa kusini.
Kuna malighafi kama vile dhahabu, urani, fosfati, kaolini, chumvi na chokaa.
HistoriaEdit
Mali ina historia ndefu ambayo ni historia ya pamoja ya nchi za kanda la Sahel na kanda la Sudan.
Zamani za Wafinisia na za Waroma palikuwa na mawasiliano ya biashara na nchi za Mediteranea kupitia wanafayabiashara Waberberi walioelewa njia za Sahara.
Uvamizi wa Wavandali katika Afrika ya Kaskazini ulivuruga mawasiliano hayo.
Baada ya uvamizi wa Waarabu na uenezaji wa Uislamu biashara ilianza upya. Ndio Waberberi Waislamu walioingiza dini mpya hata kusini ya Sahara.
Katika eneo la Mali ya leo pamoja na nchi jirani ni hasa madola matatu makubwa yaliyotawala upande wa kusini wa njia za biashara iliyovuka Sahara.
Dola la GhanaEdit
Dola la kwanza lilikuwa Dola la Ghana. Kuanzia karne ya 8 BK hadi mwaka 1076 lilitawala biashara ya dhahabu, pembe za ndovu na chumvi. Mji mkuu ulikuwa Kumbi Sale wenye wakazi 30,000 katika Mauretania ya leo.
Taarifa za wanahistoria Waarabu zimeonyesha ufalme tajiri. Utamaduni wake haukuwa wa Kiislamu bali wa Kiafrika asilia.
Mwisho wake ulianza wakati jeshi la Wamurabitun kutoka Moroko lilivuka jangwa na kuvamia Kumbi Sale.
Dola la MaliEdit
Mali ilianza kama ufalme mdogo wa Wamalinke kando ya Ghana. Wakati wa karne ya 13 ilianza kupanuka chini ya mfalme Sundiata Keita. Sundiata mwenyewe alipokea Uislamu mnamo 1240 BK na wafalme baada yake waliendela kuwa Waislamu.
Mfalme wa Mali aliyejulikana zaidi ndiye Mansa Kankan Musa I (1312–1337). Miaka 1324-1325 alihiji kwenda Makka. Alisafiri na dhahabu nyingi sana. Huku Misri alitoa zawadi kiasi cha kuharibu thamani ya dhahabu kwa miaka 12 iliyofuata.
Wakati ule mji wa Timbuktu ulikuwa kitovu cha biashara na elimu iliyojulikana kote katika umma wa Kiislamu hata Ulaya.
Katika karne ya 14 BK uwezo na utawala wa Mali ulipungua na Songhai ilichukua nafasi yake.
Dola la SonghaiEdit
Asili ya Wasonghai ilikuwa Nigeria ya Kaskazini ya leo. Walipanua utawala wao kuelekea magharibi wakapokea Uislamu wakati wa uvamizi wa Almurabitun.
Mnamo mwaka 1250 walikuwa chini ya Mali lakini katika karne ya 14 walijipatia uhuru tena, wakaanza kushika maeneo ya Mali yenyewe.
Kilele cha nguvu yake ilikuwa wakati wa mfalme Askia Mohammad I katika karne ya 16 walipotawala eneo kubwa kutoka Kano (Nigeria) hadi pwani ya Atlantiki. Wakati wake mji wa Timbuktu ilitembelewa na msafiri Leo Africanus aliyeleta baadaye habari za nchi hadi Ulaya.
Utawala wao uliporomoka baada ya mashumbulizi kutoka Moroko mwaka 1591. Wakati ule mataifa ya Ulaya yameshaanza kufika kwenye mwambao wa Afrika ya Magharibi wakifungua biashara ya moja kwa moja na Ulaya. Umuhimu wa biashara ya kuvuka Sahara ulipungua vikali pamoja na faida iliyopatikana kwa watawala katika maeneo ya Sahel.
Kipindi cha madola madogo na jihadiEdit
Kilichofuata kilikuwa kipindi cha madola madogo. Viongozi Waislamu walijaribu mara kadhaa kujenga utawala juu ya eneo lote.
Anayejulikana zaidi alikuwa Alhaj Omar aliyepiga vita kwa jina la dini ya Kiislamu dhidi ya Wabambara waliofuata utamaduni na dini asilia za Kiafrika.
Mtoto wa Alhaj Omar aliyeitwa Ahmadu alijaribu kuendeleza jihadi yake. Lakini wakati ule Wafaransa walianza kuenea katika Afrika ya Magharibi wakamshinda.
Mali ikawa koloni la Ufaransa kuanzia mwaka 1895. Ilikuwa sehemu ya Afrika ya Magharibi ya Kifaransa, na kuanzia 1920 ya Sudan ya Kifaransa.
UhuruEdit
Mwaka 1960 Mali pamoja na Senegal zilipata uhuru kama "Shirikisho la Mali". Baada ya Senegal kuacha umoja huo, Jamhuri ya Mali chini ya rais wa kwanza Modibo Keïta ikawa nchi ya kujitegemea.
Keita alipinduliwa mwaka 1968 na wanajeshi akishtakiwa kuwa ameharibu uchumi na kujitajirisha. Kiongozi mpya Moussa Traoré alitawala kama dikteta wa kijeshi, baadaye kwa msaada wa katiba ya chama kimoja.
Mabadiliko yaliyotokea kote Afrika tangu mwisho wa Ukomunisti kuanzia miaka ya 1990 yalisababisha kupinduliwa kwa Traoré katika Machi 1991 na kamati ya kijeshi iliyoongozwa na Amadou Toumani Touré.
Katiba mpya ya mwaka 1992 iliunda kipindi cha kura huru alimoshinda Amadou.
WatuEdit
Katika maeneo makubwa ya kaskazini wanaishi makabila ya Waberberi, hasa Mauri na Watuareg ambao ni wahamaji. Ndio 10% ya wakazi wa nchi wakikalia asilimia kubwa za eneo.
Kikundi kikubwa ndio Wabamana (30%) katika eneo la mji mkuu Bamako, halafu wako Wamandinka, Wafula, Wadogon, Wasonghai na wengineo.
LughaEdit
Kutokana na ukoloni, Kifaransa kimekuwa lugha rasmi. Kibambara kinaeleweka na takriban 60% za wakazi. Kwa ujumla kuna lugha 56 nchini Mali.
DiniEdit
Uislamu ni dini kubwa nchini (90 % za wakazi). Wakristo wanafikia 5% (Wakatoliki 3.3% na Waprotestanti 1.7%). Wengine wanafuata dini asilia za Kiafrika (5%).
Ibada na desturi asilia zinapatikana pia katika mazingira ya Waislamu.
Tazama piaEdit
MarejeoEdit
- Constitution of Mali (French). A student-translated English version Archived Septemba 12, 2012 at the Wayback Machine. is also available.
- DiPiazza, Francesca Davis (2006). Mali in Pictures. Minneapolis, Minnesota: Learner Publishing Group. ISBN 978-0-8225-6591-8.
- Mali country profile. Library of Congress Federal Research Division (January 2005). This article incorporates text from this source, which is in the public domain.
- Milet, Eric and Manaud, Jean-Luc (2007). Mali (in French). Editions Olizane. ISBN 2-88086-351-1.
- Velton, Ross (2004). Mali. Bradt Travel Guides. ISBN 1-84162-077-7.
Viungo vya njeEdit
- Wikimedia Atlas of Mali
- Mali entry at The World Factbook
- (Kifaransa) Serikali ya Mali tovuti rasmi
- (Kifaransa) Secrétariat Général du Gouvernement Malienne Archived Februari 22, 2016 at the Wayback Machine.
- The European Union mission in Mali - Hungary's involvement in the mission
- War at the background of Europe: The crisis of Mali
- Mali Archived Juni 7, 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Mali katika Open Directory Project
- Mali profile from the BBC News
- Mali 2012 Trade Summary Statistics
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |