Reuben Kosgei
Reuben Seroney Kosgei (Alizaliwa 2 Agosti 1979) ni mwanariadha wa Kenya wa masafa ya Kati na Masafa Marefu.
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Anawakilisha nchi Kenya | ||
Men’s Wanariadha | ||
Olympic Games | ||
Dhahabu | 2000 Sydney | 3000 m steeplechase |
World Championships | ||
Dhahabu | 2001 Edmonton | 3000 m steeplechase |
Commonwealth Games | ||
Medali ya Shaba | 2006 Melbourne | 3000 m steeplechase |
Historia
haririKazi yake ya Riadha
haririAnajulukana kwa umaarufu wake katika shindano la mita 3000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji ambapo aliwahi kuwa mshindi wa nishani ya Dhahabu mwenye umri mdogo zaidi katika Ollimpiki wakati alishinda shindano hili jijini Sydney mnamo 2000 akiwa na umri wa miaka 19 peke yake. Hata hivy, muda wake wa ushindi huo, 8:21:43 ulikuwa muda wa kasi ya chini zaidi katika hisoria ya shindano hilo tangu Mashindano ya Olimpiki ya 1972
Alikuwa mmoja wa wale waliopokea shutma kwa kukosa kushiriki katika katika Mashindano ya Jumuia ya Madola ya 2002 na badala yake wakaamua kufuata madola yaliyokuwa yameahidiwa katika Ligi ya IAAF. Wengine ni Richard Limo na Bernard Lagat.
Katika Mashindano ya Jumuia ya Madola ya 2006, hata hivyo, alishinda nishani ya Shaba katika shindano lilo hilo la mita 3000 kuruka viunzi.
Alishiriki katika shindano la Marathon kwa mara ya kwanza mnamo 2009 katika Mashindano ya Vienna Marathon lakini hakumaliza mbio hizo. Alimaliza wa pili katika Mashindano ya Florence Marathon ya 2009[1]
Mafanikio Muhimu
hariri(zifuatazo zote ni katika shindano la 3000m Kuruka Viunzi)
- 1998
- Mashindano ya Dunia ya IAAFkwa Chipukizi ya 1998 - Annecy, Ufaransa.
- Nishani ya Dhahabu
- Mashindano ya Dunia ya IAAFkwa Chipukizi ya 1998 - Annecy, Ufaransa.
- 2000
- Mashindano ya Olimpiki ya 2000 - Sydney, Australia.
- 2001
- Ubingwa wa Dunia katika riadha wa 2001 - Edmonton, Canada.
- nishani ya Dhahabu
- Michezo ya Goodwill - Brisbane, Australia.
- nishani ya Fedha
- Ubingwa wa Dunia katika riadha wa 2001 - Edmonton, Canada.
Virejeleo
hariri- IAAF wasifu wa Reuben Kosgei
- ↑ IAAF, 29 Novemba 2009: Kipruto holds off Kosgei by a second in Florence
Makala hii kuhusu Mwanariadha wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Reuben Kosgei kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii inahusu wanariadha wa Olimpiki wa Afrika bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |