Rhona Mitra
Rhona Natasha Mitra (amezaliwa tar. 9 Agosti 1976) ni mwigizaji wa filamu, mwanamitindo, na mwimbaji kutoka nchini Uingereza. Jina lake la kisanii pia kuna kipindi hujiita kama Rona Mitra.
Rhona Mitra | |
---|---|
Mitra mnamo Januari 2009 | |
Amezaliwa | Rhona Natasha Mitra 9 Agosti 1976 Paddington, London, Uingereza, UK |
Kazi yake | Mwigizaji, Mwanamitindo, Mwimbaji |
Miaka ya kazi | 1995–mpaka sasa |
Tovuti rasmi |
Maisha ya awali
haririMitra alizaliwa mjini Paddington, London, Uingereza, akiwa kama binti wa Antony Mitra, ambaye ni daktari wa upasuaji, na Nora Downey. Ana kaka'ke mkubwa, Jason Wath Mitra, ambaye ni mkubwa kwake kwa miaka miwili, na mdogo wake wa kiume.[1] Baba yake ni Mhindi-Mwingereza, na mama'ke ni Mwa-Ireland.[2][3] Mnamo mwaka wa 1984, wakati Mitra ana miaka nane, wazazi wake wakatalikiana, na yeye akapelekwa kusoma katika shule za bweni. Ametumia miaka kadhaa akijisomea katika shule mbili tofauti, ikiwemo na Roedean School, lakini Mitra anadai hatimaye alifukuzwa katika shule zote mbili.
Shughuli za uigizaji
haririMitra ameanza kujizolea umaarufu baada ya kucheza kama kipenzo cha Christopher Lambert kwenye filamu ya Beowulf hapo mnamo mwaka wa 1999. Uhusika wake mkuu umekuja kwa mara ya kwanza pale alipocheza kama kipenzi cha Scott Wolf kwenye Party of Five. Mnamo mwaka wa 2000, Mitra alipata uhusika mdogo kwenye filamu ya Hollow Man, ambapo alicheza kama yule mwanamke jirani wa Seba. Amepata kucheza kama muhusika mkuu kwenye igizo la kiafya la Gideon's Crossing, na alicheza kama Dr. Alejandra 'Ollie' Klein. Mitra pia amepa kucheza nyusika kadhaa kwenye filamu kama vile Ali G Indahouse; Sweet Home Alabama; Stuck on You, na uhusika mkuu kwenye filamu ya Highwaymen na Spartacus .
Mitra ameonekana kwenye msimu wa mwisho wa The Practice na alicheza kama Tara Wilson, na akaendelea na uhusika mwisho wake kwenye kipengele cha Boston Legal, lakini hakuendelea sana na kuondoka zake kwenye msimu wa pili.
Filmografia
haririDiscografia
haririAlbamu zake
hariri- Come Alive (1998, imetayarishwa na Dave Stewart)[4]
- Female Icon (1999, imetayarishwa na Dave Stewart)[4]
Single
hariri- "Getting Naked" (1997)[5]
Marejeo
hariri- ↑ James Mottram (2008-05-03). "Rhona Mitra: she's Mad Max in mascara for Brit thriller Doomsday". The Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-18. Iliwekwa mnamo 2008-05-03.
- ↑ Radish, Christina. "'Underworld: Rise of the Lycans' Star Rhona Mitra", MediaBlvd Magazine, 2009-01-22. Retrieved on 2009-02-01. Archived from the original on 2010-02-12.
- ↑ "The Croft Times". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-05. Iliwekwa mnamo 2009-11-16.
- ↑ 4.0 4.1 "Lara-Model als Popstar?", Spiegel Online, Spiegel-Verlag, 11 Novemba 1999. Retrieved on 8 Oktoba 2009. (German)
- ↑ "The Laras: a look back in danger", BBC News, BBC, 20 Novemba 2008. Retrieved on 8 Oktoba 2009.
Viungo vya Nje
hariri- Tovuti rasmi ya Rhona Mitra
- Rhona Mitra's Biography, News, Photos and Videos Ilihifadhiwa 13 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine. on her Birthday
- Kigezo:IMDb
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rhona Mitra kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |